Habari za Punde

Matukio ya Picha Washington DC

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akiteta jambo na Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Makao Makuu ya Shirika la Fedha la Kimataifa-IMF, Jijini Washington DC, Marekani, wakati Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan alipofanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa IMF, Bi. Kristalina Georgiva.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akiteta jambo na Mkurugenzi wa Shirika la Fedha la Kimataifa IMF anayesimamia Kanda ya Afrika Bw. Abebe Selassie, Jijini Washington DC, Marekani.
Ujumbe wa Tanzania katika mikutano ya majira ya kipupwe ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa-IMF, ukiongozwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (kulia), ukiwa nje ya jingo la Makao Makuu ya IMF, Jijini Washington DC, Marekani. Wanaofuatia ni Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Mhe. Dkt. Saada Mkuya Salum, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Emmanuel Tutuba, Kamishna wa Fedha za Nje, Wizara ya Fedha Bi. Sauda Msemo, Mshauri mwandamizi wa Mkurugenzi Mdendaji wa Benki ya Dunia kanda ya Afrika, Dkt. Zarau Kibwe na Katibu Mkuu Fedha na Mipango Zanzibar Dkt. Juma Malik Akil.

Ujumbe wa Tanzania katika mikutano ya majira ya kipupwe ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa-IMF, ukiongozwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (wan ne kushoto), ukiwa nje ya jingo la Makao Makuu ya IMF, Jijini Washington DC, Marekani.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Wizara ya Fedha na Mipango-Washington DC)

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.