Habari za Punde

Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Yakabidhi Sadaka ya Futari Futari Chuo Cha Mafunzo Zanzibar.

 MKE wa Rais wa Zanzibar ambae ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Mama Mariam Mwinyi ameushukuru uongozi wa Chuo cha Mafunzo Zanzibar kwa kukubali kupokea sadaka ya Iftar na kutaka itumike vyema kama ilivyokusudiwa.

Akizungumza na Uongozi wa Chuo cha Mafunzo katika makabidhiano ya sadaka hiyo yaliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo hicho Kilimani Jijini Zanzibar ; kwa niaba ya Mama Mariamu Mwinyi, Mjumbe wa Bodi ya Jumuiya ya Maisha Bora Foundation Jaha Haji Khamis alisema sadaka hiyo  inapaswa kutumika, walengwa wakiwa ni wanafunzi wa kike wa chuo hicho.

Alisema utoaji wa sadaka hiyo ni hatua ya utekelezaji wa azma ya Jumuiya ya kuhakikisha inatoa msukuimo katika kunyanyua maisha ya vijana na wanawake.

Nae, Mkuu wa Utawala wa Chuo cha Mafunzo Zanzibar Mrakibu Omar Hamduni Mjomba aliishukuru Jumuiya hiyo  chini ya Mwenyekiti wake Mama Mariamu kwa kuona umuhimu wa kukabidhi msaada huo.

“Kutoa ni moyo, zipo taasisi nyingi zenye uwezzo mkubwa tu na hazijafanya hivyo”, alisema.

Alisema msaada huo umekuja kwa wakati muafaka na hivyo akachukua fursa hiyo kuutaka uongozi wa Gereza kuhakikisha unatumika vyema ili kuwasaidia wnaafunzi wa kike walioko gerezani katika kipindi hiki mwezi mtukufu wa Ramadhani na sikukuu ya ya Idd el Fitr.

Aidha, aliiomba Jumuiya hiyo kufikiria uwezekano wa kutoa misaada kama hiyo kwa wanafunzi wa jinsia ya kiume, pale hali itakaporuhusu.

Miongoni mwa sadaka ya Iftari iliokabidhiwa na Jumuiya hiyo ni pamoja na Mchele, Tende, mafuta ya kupikia, maharage pamoja na chumvi.    

 

Abdi Shamna, Ikulu

Zanzibar

Postal Address: 2422 Tel.:0777476982. Fax: 024 2231822 

 E-mail: abdya062@gmail.com

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.