Habari za Punde

Msafara wa waendesha Baiskeli wa TWENDE BUTIAMA wafika Jijini Dodoma

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Bw. Juma Mkomi na viongozi wa Wizara hiyo wakiwa katika picha ya pamoja na waendesha baiskeli wa Twende Butiama katika Ofisi za Wizara hiyo zilizopo mtumba Jijini Dodoma.
Msafara wa Baiskeli wa Twende Butiama ukiwasili katika Ofisi za Wizara ya Maliasili na Utalii zilizopo mji wa Serikali, Mtumba Jijini Dodoma. Msafara huo wa waendesha baiskeli hao unaelekea Butiama katika kuadhimisha miaka 100 ya Hayati Julius Kambarage Nyerere
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Bw. Juma Mkomi akizungumza na Mkuu wa Msafara wa Baiskeli wa Twende Butiama Bw. Gabriel Landa wakati msafara huo ulipowasili katika Ofisi za Wizara hiyo zilizopo mji wa Serikali, Mtumba Jijini Dodoma ukielekea Butiama, Mkoani Mara katika kuadhimisha miaka 100 ya hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Waendesha Baiskeli wa Twende Butiama wakiwa pamoja wasanii wa kikundi cha Julius Nyerere Festival wakiimba nyimbo za hamasa mara baada ya kuwasili katika Ofisi za Wizara ya Maliasili na Utalii zilizopo mji wa Serikali, Mtumba Jijini Dodoma leo Jijini Dodoma
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Bw. Juma Mkomi akitia saini ikiwa ni ishara ya waendesha baiskeli hao kufika Jijini Dodoma.

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.