Habari za Punde

"NIKO Tayari Kufanya Kazi Muda Wowote Mhe.Pindi Chana.

 

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana (Mb) akizungumza  na menejimenti ya Wizara ya Maliasili na Utalii mara baada ya kuripoti ofisini Mtumba jijini Dodoma baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.  Kushoto ni aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye kwa sasa ni Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb).

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana ameahidi kushirikiana na watendaji na watumishi wa Wizara yake katika kutekeleza majukumu mbalimbali ya Wizara hiyo.

Ameyasema hayo leo Aprili 2,2022 alipowasili katika ofisi za Wizara ya Maliasili na Utalii zilizopo Mtumba jijini Dodoma mara baada ya kuapishwa.

“Niwahakikishie kwamba niko tayari kuchapa kazi pamoja nanyi,  imani kubwa ambayo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ametupa hatutamuangusha” Mhe. Chana amesisitiza.

Aidha, ameweka bayana kuwa yuko tayari kufanya kazi kwa saa 24 bila kikwazo chochote. 

"Mimi kama  Waziri  wenu  milango iko wazi saa 24, hakuna wakati sitapatikana iwe ni usiku, iwe asubuhi hata iwe sikukuu na ndio maana ya kuwa mtumishi wa umma.” Amesisitiza.

Naye, Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) ameeleza kuwa Wizara imepata mtu sahihi wa kuitoa ilipo na kuisogeza mbele na kwamba Mhe. Pindi Chana yuko na timu ya watendaji mahiri na wachapakazi. 

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) amemkaribisha Waziri Pindi Chana na kumpongeza kwa kuteuliwa kushika wadhifa huo.

“Tunakukaribisha sana katika Wizara ya Maliasili na Utalii na kukupongeza sana kwa kuteuliwa kushika wadhifa wa Waziri wa Maliasili na Utalii”amesema Mhe. Masanja 

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana ameanza kazi leo kwa mara ya kwanza mara baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana (Mb) (kushoto) akisalimiana na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) mara baada ya kuripoti ofisini Mtumba jijini Dodoma baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana (Mb) (kushoto) akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Juma S. Mkomi (kulia) mara baada ya kuripoti ofisini Mtumba jijini Dodoma baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan. Katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Francis Michael na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb).
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana (Mb) akisalimiana na watumishi mara baada ya kuripoti ofisini Mtumba jijini Dodoma baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan. Kulia ni aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye kwa sasa ni Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) na kushoto ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb).
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Francis Michael akizungumza wakati wa kikao cha Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana (Mb) (wa pili kutoka kushoto) na menejimenti ya Wizara hiyo mara baada ya Waziri kuripoti ofisini Mtumba jijini Dodoma baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan. 
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) akimpongeza na kumkaribisha Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana (Mb) (wa pili kutoka kushoto) mara baada ya kuripoti ofisini Mtumba jijini Dodoma baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan. Kushoto ni aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye kwa sasa ni Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Francis Michael (kulia).
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana (Mb) akikabidhiwa nyaraka mbalimbali kama ishara ya kukabidhiwa ofisi na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Francis Michael (kulia) mara baada ya kuripoti ofisini Mtumba jijini Dodoma baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan. Wanaoshuhudia ni aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye kwa sasa ni Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) (kushoto) na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb)(wa pili kutoka kulia).
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana (Mb) akizungumza  na menejimenti ya Wizara ya Maliasili na Utalii mara baada ya kuripoti ofisini Mtumba jijini Dodoma baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.