Habari za Punde

OMOLO: MKAFANYE KAZI WA KUSHIRIKIANA ILI KULETA MAENDELEO YA CHUO

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Jenifa Christian Omolo, akizungumza wakati wa halfa ya uzinduzi wa Bodi ya Wakurugenzi ya Chuo Cha Takwimu Mashariki Mwa Afrika, iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Chuo Cha Takwimu Mashariki Mwa Afrika Dkt. Tumaini Katunzi, akitoa maelezo kwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Jenifa Christian Omolo, alipotembelea chuoni hapo wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi hiyo jijini Dar es Salaam.

Na.Josephine Majura WFM, Dar es Salaam

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Jenifa Omoloameitaka Bodi ya Wakurugenzi ya Chuo Cha Takwimu Mashariki Mwa Afrika, kuhakikisha inatekeleza majukumu yake  kwa weledi ili Chuo hicho kupiea hatua zaidi kimaendeleo kwa kuboresha miundombinu na masuala ya taaluma.

 

Bi. Omolo alitoa wito huo wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi ya Wakurugenzi ya  Chuo Cha Takwimu Mashariki Mwa Afrika, uliofanyika katika ukumbi wa Chuo hicho jijini Dar es Salaam.

 

“Tuna imani na ninyi na nimatumaini yetu mtatumia uzoefu wenu, maarifa na weledi katika kutekeleza majukumu yenu kwa manufaa ya Chuo na Taifa kwa ujumla”, aliongeza Bi. Omolo.

Aidha, alilitaka Bodi hiyo ishirikiane na Menejimenti ya Chuo, Watumishi na Wadau wa Takwimu ili  kuhakikisha Chuo kinatekeleza majukumu yake kupitia  mpango mkakati waliojiwekea ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Bi. Omolo aliitaka Bodi hiyo kushirikiana na Menejimenti ili kuhakikisha wanaimarisha mahusiano mema na nchi wanachama na wadau walio ndani na nje ya nchi.

Sambasamba na uzinduzi wa Bodi hiyo Bi. Omolo alitembelea maeneo ya Chuo hicho ambapo alijonea miundombinu mbalimbali chuoni hapo, na aliitaka Bodi hiyo kubaini na kuainisha changamoto zinazokikabili na kuzifanyia kazi mapema kabla ya kuleta athari katika utoaji wa huduma chuoni hapo.

Alimpongeza Mwenyekiti wa Bodi hiyo ya Wakurugenzi Prof. Ahmed Ame kwa kuteuliwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  kuwa Mwenyekiti wa Bodi hiyo na kuwapongeza Wajumbe wa Bodi kwa  kuteuliwa na Waziri wa Fedha na Mipango.

Kwa upande wake Mwenyekiti Bodi ya Chuo Cha Takwimu Mashariki Mwa Afrika Prof. Ahmed Ame, alimhakikishia Naibu Katibu Mkuu, kuwa Bodi hiyo itafanya kazi kwa weledi mkubwa ili kuhakikisha malengo waliyojiwekea yanafikiwa kwa wakati.

“Nikuhakikishie Mheshimiwa Mgeni rasmi hii ni Bodi ya Takwimu hivyo nikutoe wasiwasi tutakuwa tunafanya tathimini kila mwaka kupitia takwimu mbalimbali tutakazokuwa tunatoa”, alisisitiza Prof. Ame.

Katika hatua nyingine alifanya kikao na Menejimenti ya Chuo hicho ambapo aliiagiza Menejimenti hiyo kukitangaza Chuo chao ili kuongeza udahili wa wanafunzi kutoka ndani na nje ya nchi kwa kuwa Chuo hicho kina hadhi ya Kikanda kikihudumia nchi 19 za Afrika zinazotumia lugha ya kiingereza.

“Nitumie nafasi hii pia kuwakaribisha kwenye familia ya Wizara ya Fedha na Mipango.  na matarajio yangu mtatekeleza majukumu yenu kwa ushirikiano wa karibu na Wizara pamoja na Taasisi nyingine ili kuhakikisha mipango tuliyojiwekea inafikiwa”, alisema Bi Omolo”.

Naye Mkuu wa Chuo Cha Takwimu Mashariki Mwa Afrika Dkt. Tumaini Katunzialisema kuwa Menejimenti ya Chuo hicho itatekeleza maelekezo yote yaliyotolewa ili kuhakikisha shughuli za maendeleo zinafikiwa chuoni hapo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.