Habari za Punde

Hospitali ya Uhuru Chamwini Mkoani Dodoma Yapongezwa.

 

Muonekano wa jengo jipya la Hospitali ya Uhuru ya Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma 

Na.Adeladius Makwega-DODOMA

Kanisa Katoliki limeipongeza Hospitali ya Uhuru ya Wilayani Chamwino mkoani Dodoma iliyopo kandakando ya Barabara inayokwenda Morogoro njia ya panda ya kuingia Chamwino Ikulu kwa kuhudumia wagonjwa vizuri wanapofika hapo kutibiwa.

Hayo yamesemwa na Paroko wa Kanisa la Bikira Maria Imakulata Chamwino Ikulu Jimbo Kuu katoliki la Dodoma Paul Mapalala katika matangazo mwishoni mwa misa ya kwanza ya dominika ya Mei 15, 2022 inayoanza saa 12 ya asubuhi ya kila jumapili.

“Nilikwenda hospitalini hapo nikiwa mgonjwa sana, siku ya ijumaa na kweli madaktari, wauguzi na watumishi wa hospitali hii walinipokea vizuri sana, wakanipatia vipimo, nikapatiwa dawa na huku wakifika kunijulia hali hadi sasa nimepona kabisa.”

Moyo huu wa ukarimu kwa wagonjwa ni moyo mwema sana nimeona nilivyotendewa mimi na wakitendewa wengine hospitalini hapo kwa maana mgonjwa anapoumwa anahitaji faraja kubwa kwanza kwa wahudumu wa afya na pili kwa jamii yake alipo, alisema.

“Ninawashukuru mno hata waamini kadhaa waliojitokeza kuniona katika ugonjwa wangu hilo ni jambo jema na hiyo ndiyo imani yetu.” Alisisitiza Paroko Mapalala.

Hospitali ya Uhuru ni miongoni mwa hospitali kubwa za serikali katika mkoa Dodoma ambayo ipo katika Wilaya ya Chamwino kilomita kadhaa kutoka ilipo Ikulu ya Chamwino ambayo inato ahuduma mbalimbali za tiba.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.