Habari za Punde

Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan atembelea eneo la Makumbusho na kuweka Shada la maua katika Kaburi la Rais wa kwanza wa Ghana Kwame Nkrumah, Accra nchini Ghana

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na viongozi mbalimbali pamoja na Wafanyakazi wa Sekretarieti ya Mkataba wa eneo huru la Biashara Barani Afrika (The African Continental Free Trade Area), katika Ofisi za (AfCFTA)  Jiji la Accra nchini Ghana tarehe 25 Mei, 2022.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Katibu Mkuu wa Wamkele Mene katika Ofisi za (AfCFTA) Accra nchini Ghana
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiweka Shada la Maua kwenye Kaburi la aliyekuwa Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Ghana Hayati Dkt. Kwame Nkrumah wakati alipotembelea eneo la Makumbusho (Kwame Nkrumah Memorial Park and Mausoleum) katika Jiji la Accra nchini Ghana
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiweka Shada la Maua kwenye Mnara wa kumbukumbu katika eneo la Makaburi alipozikwa aliyekuwa Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Ghana Hayati Dkt. Kwame Nkrumah wakati alipotembelea eneo la Makumbusho (Kwame Nkrumah Memorial Park and Mausoleum) katika Jiji la Accra nchini Ghana

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.