Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akitoa maelekezo kwa mkandarasi anayejenga Daraja la Nyeburu Mhandisi Mussa Miraji wa kampuni ya Giraf Investment kuhakikisha daraja hilo linalounganisha Pugu na Chanika linakamilika kwa wakati. (Pembeni ni mhandisi matengenezo wa TANROADS mkoa wa Dar es salaam Eliseus Mtenga )

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akisikiliza maelezo kutoka kwa mhandisi matengenezo wa TANROADS mkoa wa Dar es salaam Eliseus Mtenga wakati aliposimama katika Daraja linalojengwa la Nyeburu linalounganisha Pugu na Chanika tarehe 17 Juni 2022.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango amewaasa
wakandarasi wazawa kutumia vema na kwa ufanisi fursa wanazopewa na serikali za
ujenzi wa miradi mbalimbali ili kuendelea kupewa nafasi hizo zaidi.
Makamu
wa Rais amesema hayo wakati aliposimama na kukagua ujenzi wa daraja la Nyeburu
linalounganisha eneo la Pugu na Chanika Jijini Dar es salaam ambalo ujenzi wake
umekuwa ukisuasua. Makamu wa Rais ameonesha kutofurahishwa na maendeleo ya
ujenzi huo ambapo amaesema ujenzi wa daraja hilo umechukua muda mrefu na kutoa
athari kwa wananchi hasa wakati wa mvua licha ya serikali kuendelea kutoa
malipo kwa wakati kwa mkandarasi katika kila kazi.
Aidha
Makamu wa Rais amesema serikali imeendelea kuwapa kipaumbele wakandarasi wa
ndani kutokana na kutambua wanafahamu vema changamoto zinazosababishwa na ubovu
wa miundombinu hivyo wanapaswa kutekeleza majukumu yao kiufanisi zaidi.
Pia Makamu wa Rais amewataka wakala wa barabara mijini na vijijini (TARURA) pamoja na TANROADS kuwasimamia kikamilifu wakandarasi ili wakamilishe miradi kwa wakati na kuokoa fedha za walipa kodi wa Tanzania.
No comments:
Post a Comment