Habari za Punde

Waziri wa Wizara ya Fedha na Mipango Mhe.Dkt.Mwingulu Nchemba Awasilisha Hutuba ya Bajetri ya Wizara ya Fedha na Mipando 2022/2023

Mheshimiwa Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akiwasilisha Bungeni Jijini Dodoma, Makadirio ya Mapato na Matumizi ambapo ameliomba Bunge kuiidhinishia Wizara yake Bajeti ya shilingi trilioni 14.94 (sh. tril 13.62 matumizi ya kawaida na sh. tril 1.32 matumizi ya maendeleo) kwa mafungu yake 8 kwa ajili ya matumizi ya kawaida na maendeleo kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023

Viongozi na Wakuu wa Taasisi zilizochini ya Wizara ya Fedha na Mipango wakifuatilia uwasilishwaji wa Bajeti ya Wizara uliofanywa na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), aliyewasilisha Bungeni Jijini Dodoma, Makadirio ya Mapato na Matumizi ambapo ameliomba Bunge kuiidhinishia Wizara yake Bajeti ya shilingi trilioni 14.94 (sh. tril 13.62 matumizi ya kawaida na sh. tril 1.32 matumizi ya maendeleo), kwa mafungu yake 8 kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango)

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.