Habari za Punde

Mmuya Aridhishwa nas Ujenzi wa Kituo cha Uratibu na Udhibiti wa wa Maafa Nchini.


Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu) Bw.Kaspar Mmuya akitoa maelekezo alipotembelea na kukagua Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha Maafa katika eneo la ujenzi Nzuguni B Jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu) Bw.Kaspar Mmuya (katikati) akikagua Ramani ya Mradi wa Kituo cha Uratibu na Maafa katika eneo la ujenzi Nzuguni B Jijini Dodoma
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu) Bw.Kaspar Mmuya alipokagua Ujenzi wa Msingi wa Jengo la Mradi wa Kituo cha Uratibu na Maafa katika eneo la ujenzi Nzuguni B Jijini Dodoma.
Mkadiriaji wa Majengo Sauden Anania akitoa taarifa kwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu) Bw.Kaspar Mmuya ya maendeleo , Mradi ujenzi wa Kituo cha Uratibu na Maafa katika eneo la ujenzi Nzuguni B Jijini Dodoma.

                     (PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

Na Mwandishi wetu - Dodoma

Naibu katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu)   Bw. Kaspar Mmuya ametembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa kituo cha Uratibu na Maafa unaoendelea katika eneo la Ujenzi la Nzuguni B Jijini Dodoma unaogharimu Zaidi ya Bilioni mbili.

Akizungumza mara baada ya kukagua ujenzi huo Naibu katibu Mkuu Kaspar Mmuya amesema Ofisi yao  inasimamia ubora wa shughuli, Thamani ya Fedha  pamoja na spidi ya ujenzi wa miradi  hivyo licha ya changamoto ndogondogo zilizopo katika mradi huo ni vizuri mkandarasi akaongeza spidi ya ujenzi wa mradi huo.

“Ni vizuri kutumia kipindi ambacho hakina changamoto nyingi kufanya kazi nyingi  kwa uharaka ili changamoto zikija zile ambazo huwezi kuzikabili inakuwa rahisi ambapo umeshafika sehemu ya juu kwa hiyo mimi wito wangu ni kuongeza spidi maana kuongeza spidi ni jambo la kawaida tu ni kuongeza nguvu kazi , kuongeza vifaa ,unaongeza muda wa kazi basi”.

Aidha Mmuya ameahidi kurudi kutembelea mradi huo ndani ya mwezi mmoja na kumtaka Mkadiriaji wa Majengo  Sauden Anania kuhakikisha anampa taarifa ili kushirikiana na ofisi yake na kuifanya kazi kuwa rahisi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.