Habari za Punde

Khatib Haji Khamis Aibuka Mshindi wa Mashindano ya Ngalawa ya "CRDB Ngalawa Race"

Sehemu ya Ngalawa zilizoshiriki katika mashindano ya ‘CRDB Bank Ngalawa Race' yaliyoandaliwa na Benki ya CRDB katika Tamasha la Kizimkazi, yaliyofanyika leo Agosti 30, 2022 kwenye fukwe za Kizimkazi Mkunguni, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar.
Sehemu ya Ngalawa zilizoshiriki katika mashindano ya ‘CRDB Bank Ngalawa Race' yaliyoandaliwa na Benki ya CRDB katika Tamasha la Kizimkazi, yaliyofanyika  Agosti 30, 2022 katika fukwe wa bahari ya Kizimkazi Mkunguni Wilaya ya Kusini  Mkoa wa Kusini Unguja Zanzibar.
Washiriki wa mashindano ya Ngalawa ya ‘CRDB Bank Ngalawa Race' yaliyoandaliwa na Benki ya CRDB katika Tamasha la Kizimkazi, wakiaza mashindano hayo yaliyofanyika  Agosti 30, 2022 kwenye fukwe za Kizimkazi Mkunguni, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar.

Mshindi wa kwanza wa mashindano ya Ngalawa ya ‘CRDB Bank Ngalawa Race' Ndg. Khatib Haji Khamis akimaliza mashindano hayo kwa kuibuka mshindi akiwasili katika ufukwe wa bahari ya Kizimkazi Mkunguni  wakati wa Tamasha la Kizimkazi lililofanyika Mkoa wa Kusini Unguja na kuandaliwa na Benki ya CRDB Bank 

Mshindi wa kwanza wa CRDB Ngalawa Race, Khatib Haji Hamis akiwa juu ya boti iliyokabidhiwa zawadi kwa kijiji chake cha Kizimkazi Mkunguni kwa ajili ya kuchochea maendeleo. Boti hiyo ina thamani ya shilingi milioni 25.
Wananchi Kizimkazi na Mkoa wa Kusini Unguja wakishangilia wakati wa kuwasili mshindi wa kwanza wa mashindindo ya CRDB Bank Race Ngalawa Ndg.Khatib Haji Khamis akiwasili katika ufukwe wa bahari ya kizimkazi kwa kumalizia mashindano hayo ikiwa ni Tamasha la Kizimkazi lililoandaliwa na Benki ya CRDB.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.