Habari za Punde

Mhe Hemed avishukuru vyombo vya habari kuhamasisha sensa ya Watu na Makazi

Kaimu Mkurugenzi Uhuru FM Ndg. Amina Aziz akieleza mafupi katika Bonanza lililoandaliwa na Uhuru Fm na Bahari FM chini ya Chama Cha Mapinduzi Uwanja wa Mnara wa Kumbukumbu ya Mapinduzi Muembe Kisonge lenye lengo la kuhamasisha Zoezi la Sensa ya Watu na Makazi
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar akiongozi matembezi ya Wananchi na Viongozi mbali mbali katika Bonanza la mazoezi lenye lengo la Kuhamasisha Zoezi la Sensa ya Watu na Makazi yaliloanzia Uwanja wa Amani Nje na kumalizia  Uwanja wa Mnara wa Kumbukumbu ya Mapinduzi Muembe Kisonge lenye lengo la kuhamasisha Zoezi la Sensa ya Watu na Makazi.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akimvisha Medali Mshindi wa Kwanza wa Mbio za Riadha wanawake Ramla Fabian kutoka JKU katika Bonanza lililoandaliwa na Uhuru Fm na Bahari FM chini ya Chama Cha Mapinduzi Uwanja wa Mnara wa Kumbukumbu ya Mapinduzi Muembe Kisonge lenye lengo la kuhamasisha Zoezi la Sensa ya Watu na Makazi.


Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akivisha Medali Mshindi wa Kwanza wa Mbio za Riadhaa Wanaume Nelson Liva kutoka JKU katika Bonanza lililoandaliwa na Uhuru Fm na Bahari FM chini ya Chama Cha Mapinduzi Uwanja wa Mnara wa Kumbukumbu ya Mapinduzi Muembe Kisonge lenye lengo la kuhamasisha Zoezi la Sensa ya Watu na Makazi.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akipongeza Ndugu Abdul Khatib  Abdul mwenye Mahitaji Maalum baada ya kumvisha medali ya kushriki Mbio za Riadha Kilo mita 10 katika Bonanza lililoandaliwa na Uhuru Fm na Bahari FM chini ya Chama Cha Mapinduzi Uwanja wa Mnara wa Kumbukumbu ya Mapinduzi Muembe Kisonge lenye lengo la kuhamasisha Zoezi la Sensa ya Watu na Makazi.
 

Na Abdulrahim Khamis, OMPR

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amevishukuru Vyombo vya Habari Nchini kwa Jitihada zao za kuhamasisha na Kushajihisha Sensa inayotarajiwa kufanyika Nchini Agosti 23 Mwaka huu.

 

Mhe. Hemed ameeleza hayo katika Mbio za Uhamasishaji wa Sensa zilizoandaliwa na Kituo cha Radio Uhuru FM kwa kushirikiana na Bahari Fm Radio zilizoanzia Uwanja wa Amani Nje na kumalizia Uwanja wa Mnara wa Kumbukumbu  ya Mapinduzi Michenzani Jijini Zanzibar.

 

Amesema Vyombo vya Habari vina Jukumu la Kutoa Elimu kwa Wananchi juu ya Masuala mbali mbali ya Kijamii ambapo Watanzania wanashuhudia namna Vyombo hivyo vinavyoendelea na Uhamasishaji wa Zoezi la Sensa.

 

Amesema kitendo cha Uhuru FM kuungana na Bahari FM katika kuandaa Mbio hizo ni la kupigiwa Mfano kwa kuona Umuhimu wa kushirikiana na Jamii ili kuhakikisha Ujumbe unafika Haraka.

 

"Binafsi nimefurahishwa sana kuona Uhuru FM na Bahari Fm kuandaa Mbio hizi mlikuwa na uwezo wa kuendelea kuelimisha kupitia Radio lakini mkaona bado haitoshi na inalazimika tushirikiane na Jamii husika ili kuhakikisha Ujumbe huu unafika haraka. Hongereni Sana" Mhe. Hemed

 

 

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amesema Uelimishaji na Uhamasishaji kuhusu Sensa ni suala la Msingi kutokana na baadhi ya Wanajamii wanaamini kuwa Kuhesabiwa ni Balaa na Nuksi na kutaka Jamii kuendelea kuelimisha ili wenye fikra hizo waweze kufahamu Zaidi umuhimu wake.

 

"Uelimishaji na uhamasishaji ni lazima kupewa kipaumbele  kwa sababu ndani ya Jamii yetu tuna suala zima la Mila na Desturi, kuna wale wanaoamini kuhesabiwa ni Balaa na Nuksi, eti kusema una watoto wangapi ni vibaya, eti utafikwa na Maafa ,tuendelee kuelimishana" Amesema Mhe. Hemed

 

 

Sambamba na hayo Mhe. Hemed ametoa Wito kwa  Jamii kutowaficha Watu Wenye Ulemavu na Makundi Maalum wakati wa kuhesabiwa ikiwa nao ni katika Jamii ili Serikali iweze kujua Stahiki zao.

 

"Na Katika hili naomba nitoe Wito kwa Watu wenye Ulemavu washiriki kwa Ukamilifu wake na wala wasifichwe" Amesema Mhe. Hemed

 

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amewataka Wananchi kutoa Mashirikiano ya kutosha kwa Makarani watakaofika katika maeneo yao wakati wa kuhesabiwa na kuhakikisha wanatoa Taarifa Sahihi.

 

Pamoja na hayo Mhe. Hemed amesema Serikali inahitaji Idadi Sahihi ya Wananchi wake ambazo zitakuwa ni muongozo wa Utoaji wa Huduma Nchini.

 

Mhe. Hemed ametumia Fursa hiyo kuwataka wananchi kudai na kutoa Risiti wanapofanya Miamala na kueleza kuwa zoezi hilo ni la Lazima na sio Hiari na kueleza kuwa Serikali imejipanga kufanya Mabadiliko ya Kiuchumi hivyo, ni Wajibu kukusanya Mapato ili kuyapata Mabadiliko hayo.

 

Nae Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar Dkt. Abdallah Juma Sadala ameeleza kuwa Chama Cha Mapinduzi kinathamini Juhudi za Serikali kwa kuisimamia Ilnai ya Uchaguzi ya CCM ya 2020-2025 na kueleza kuwa Zoezi la Sensa ni suala la Kitaifa kwa Maslahi ya Wananchi wake.

 

Aidha Dkt. Mabodi amewataka Wanachama wa Chama cha Mapinduzi kuendelea kudai na Kutoa Risiti wanapofanya Miamala ya kibiashara na kueleza kuwa baada ya kukamilika kwa Zoezi la Sensa Serikali inajipanga kuwaletea maendeleo Wananchi wake.

 

"Wananchi waelewe ukishapanga lazima Upange Maendeleo, na Maendeleo yanayohitaji Mapato.  Hivyo, todai na kutia Risiti tena za Kielektroniki" Amesema.

 

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Uhuru FM Amina Aziz ameeleza kuwa Lengo la kuandaa Mbio hizo ni  kuunga Mkono Juhudi za Serikali katika kuwatumikia Wananchi wake kwa kuona Umuhimu wa Kushajihisha Zoezi la Sensa kupitia Mbio hizo.

 

Ameeleza kuwa Uhuru FM wameandaa vipindi mbali mbali vya kuhamasisha Zeozi la Sensa ikiwemo vidokezo, Makala na Vipindi Maalum ili kurahisisha uelewa wa Sensa kuwafikia Wananchi wengi.

 

Mbio hizo zimejumuisha Amsha Amsha ya Matembezi pamoja na Mazoezi ya Viungo, Riadha Wanaume na Wanawake, Matembezi ya Watu wenye Ulemavu, Watembea kwa Baskeli Mikoa yote ya Unguja kwa Saa Tatu.

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.