Habari za Punde

Rais Dk Hussein Mwinyi ashiriki zoezi la sensa ya watu na makaazi

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakimsikiliza Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makaazi Zanzibar Balozi.Mohammed Hamza, kabla ya kuanza kwa zoezi lililofanyika katika Makazi ya Rais Ikulu Ndogo Migombani Wilaya ya Mjini Unguja leo 23-8-2022, na (kushoto kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Idrisa Kitwana Mustafa.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi, wakimsikiliza Karani wa Sensa ya Watu na Makazi Bi.Asia Hassan Mussa  wakati wa zoezi la kuhesabiwa lililofanyika katika makaazi yake Migombani Ikulu Ndogo leo 23-8-2022, zoezi hilo la Sensa ya Watu na Makazi lilioza leo kwa pande zote mbili za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar (hawapo pichani) baada ya kumaliza zoezi la kuhesabiwa la Sensa ya Watu na Makazi lililofanyika leo 23-8-2022, katika makazi yake Migombani Ikulu Ndogo Wilaya ya Mjini Unguja.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na kuagana na Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi Zanzibar Balozi Mohammed Hamza na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Idrisa Kitwana Mustafa, baada ya kumalizika kwa zoezi la kuhesabiwa la Sensa ya Watu na Makazi lililofanyika katika makazi yake Migombani Ikulu Ndogo leo 23-8-2022.
(Picha na Ikulu)
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.