Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi Amtembelea Mzee Khamis Abdulla Ameir Aliyewahi Kuwa Mjumbe wa Baraza la Kwanza la Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Mzee Khamis Abdulla Ameir aliyewahi kuwa Mjumbe wa Baraza la Kwanza la Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, alipofika nyumbani kwake Maisara kumtembelea na kumjulia hali yake
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akikabidhiwa  Kitabu kinachoelezea Historia ya Maisha yake Mzee Khamis Abdulla Ameir, aliyewahi kuwa Mjumbe wa Baraza la Kwanza la Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, baada ya kumaliza mazungumzo alipofika nyumbani kwake Maisara Wilaya ya Mjini Unguja kwa ajili ya kumjulia hali yake leo 12-8-2022
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akisoma Kitabu kilichoandikwa na Mzee Khamis  Abdulla Ameir, kinachozungumzia historia yake, baada ya kukabidhiwa wakati wa mazungumzo yao alipofika nyumbani kwake Maisara  Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar kumtembelea na kumjulia hali yale leo 12-8-2022.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiagana na Mzee Khamis Abdulla Ameir, aliyewahi kuwa Mjumbe wa Baraza la Kwanza la Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, baada ya kumaliza mazungumzo yao alipofika nyumbani kwake Maisara Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar  kumtembelea na kumjulia hali yake leo 12-8-2022.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.