Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj.Dk.Hussein Ali Mwinyi Ashiriki Katika Maziko ya Mke wa Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais.Donge.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein  Ali Mwinyi akijumuika na Wananchi katika kupokea jeneza likiwa na mwili wa Marehemu Hamida Mussa Omar. Mke wa Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Ndg.Faina Idarous  (kushoto kwa Rais) na Kulia kwa Rais) Naibu Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh. Mahmoud Mussa Wadi, kwa ajili ya kusalia, Sala hiyo iliyofanyika katika Msikiti Mkuu wa Ijumaa Donge Karange Mkoa wa Kaskazini Unguja
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akijumuika na Waumini wa Dini ya Kiislam katika Ibada ya Sala ya jeneza ikiongozwa na Naibu Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Mahmoud Mussa Wadi, iliyofanyika katika Msikiti Mkuu wa Ijumaa Donge Karange Mkoa wa Kaskazini Unguja leo 7-8-2022. na (kushoto kwa Rais) Mume wa Mareheme Hamida Mussa Omar, Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Ndg. Faina Idarous, Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla. na (kulia kwa Rais) Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Hassan Othman Ngwali na Makamu wa Kwanza wa Rais Mhe. Othman Masoud Othman.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akijumuika na Waumini wa Dini ya Kiislam wakiitikia dua ikisomwa na Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Hassan Othman Ngwali.(kulia kwa Rais) baada ya kumalizika kwa Ibada ya Sala ya jeneza , iliyofanyika katika Msikiti Mkuu wa Ijumaa Donge Karange Mkoa wa Kaskazini Unguja leo 7-8-2022. na (kushoto kwa Rais) Mume wa Mareheme Hamida Mussa Omar, Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Ndg. Faina Idarous, Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akiweka mchanga katika kaburi la Marehemu Hamida Mussa Omar, wakati wa maziko yake yaliofanyika Kijijini kwao Donge Karange Mkoa wa Kaskazini Unguja leo 7-8-2022
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akishiriki katika kuitikia dua ya kumuombea Marehemu Hamida Mussa Omar, baada ya kumalizika kwa maziko hayo yaliyofanyika katika Kijiji cha Donge Karange Mkoa wa Kaskazini Unguja leo 7-8-2022, na (kulia kwa Rais) Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Alhaj Othman Masoud Othman na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe, Ayoub Mohammed Mahmoud na (kushoto kwa Rais) Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhaj. Hemed Suleiman Abdulla.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi  akitowa mkono wa Pole kwa familia ya Marehemu Hamida Mussa Omar, Mke wa Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Ndg. Faina Idarous (kulia kwa Rais) alipofika nyumbani kwa marehemu Donge Karange  na (kushoto kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud  
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi  akijumuika na Familia ya Marehemu Hamida Mussa Omar, wakiitikia dua ya kumuombea Marehemu Hamida Mussa Omar, ikisomwa na Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Hassan Othman Ngwali(hayupo pichani) baada ya kutowa mkono wa Pole kwa familia alipofika nyumbani kwa marehemu Donge Karange Mkoa wa Kaskazini Unguja.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.