Habari za Punde

Watanzania Tuendelee Kuwa Wazalendo -- MAJALIWA

 

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida, katika ukumbi wa Chuo cha Uhasibu (TIA) wakati alipohitimisha ziara ya siku mbili mkoani SingidaAgosti 6, 2022.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Watanzania waendelee kuwa wazalendo kwa Taifa lao na washirikiane na Serikali katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

 

Ametoa kauli hiyo jana (Ijumaa, Agosti 05, 2022) wakati akizungumza na wakazi wa Ikungi alipokuwa katika ziara ya kikazi kataka wilaya ya Ikungi mkoani Singida.

 

“Nataka niwasihi msikwamishe maendeleo, lazima kila mmoja awe na uzalendo na wilaya yake, nawapongeza madiwani kwa mpango wenu wa kupanga mji huu.”

 

Waziri Mkuu alisema halmashauri ya wilaya hiyo imeweka mpango wa kuendeleza mji wake, wananchi ambao maeneo yao yatachukuliwa kupisha mradi huo watafidiwa kulingana na taratibu za uthamini.

 

Alisema Mthamini wa Serikali ana vigezo vya fidia, hivyo aliwasihi wananchi hao kuacha tabia ya kukataa kila mthamini anayekwenda kufanya uthamini katika eneo lao.

 

“Lazima mthamini mipango ya halmashauri yenu ya kuuboresha mji huu, isitokee mtu mmoja au wawili wakakwamisha maendeleo ya wenzao wa wilaya nzima.”

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.