Habari za Punde

Maadhimisho ya Siku ya Afya ya Akili Duniani “Kuifanya Afya ya Akili Kuwa na Manufaa kwa Wote”

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar Mhe, Saada Mkuya Salum akiwahutubia wadau mbalimbali wa Afya katika maadhimisho ya siku ya Afya ya Akili Duniani yaliofanyika huko Hospitali ya Magonjwa ya Akili Kidongochekundu Zanzibar.

Na Rahma Khamis Maelezo Zanzibar                             

Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi ameitaka jamii kuendelea kwenda vituo vya Afya pindi wanapopatwa na tatizo la Afya ya Akili ili kuweza  kupatiwa tiba .

Wito huo ameutoa katika Viwnja vya Hospitali ya maogonjwa ya akili Kidongochekundu wakati akiwahutubia wananchi katika kilele cha maadhimisho ya siku ya Afya ya Akili Duniani.

Akizungumza kwa niaba, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar Mhe, Saada Mkuya Salum amesema kuwa akili ni nyenzo muhimu kwa mwanadamu ambayo hutumia katika kufanya mambo yake hivyo ikitokea kuwa viashiria vya tatizo hilo ni vyema kuwahi kufika Hospitali mapema kuliko kutumia dawa nyengine.

Amesema kuwa kuna baadhi ya watu wanawanyanyapaa na kuwabagua wagonjwa wa afya ya akili jambo amblo ni kinyume na utaratibu kwa vile na wao wana haki kama watu wengine.

“Unyanyapaa na ubaguzi unaendelea kuwa tatizo kwa wagonjwa wa akili hivyo tuhakikishe kuwa tunawapatia matunzo wgonjwa wetu ili na wao wajisikie kuwa wanathaminiwa katika jamii yetu,”alisema Mama Mariam.

Aidha amefahamisha kuwa  Zanzibar ina zaidi ya wagonjwa  asilimia 6.8 kwa makisio ambao wanaishi na tatizo la afya ya akili kwa watu wazima ,wanaume na wanawake jambo ambalo ni la kushtusha hivyo ipo haja kwa jamii kupatiwa elimu kuhusu tatizo hilo.

“Wakati tutapopata takwimu sahihi ya matokeo ya sensa tutaweza kupata idadi kamili ya wagonjwa wa afya ya akili na kuweza kufanya mikakati ya kupata madawa na mambo mengine kw uhakika”, Mama Mariam alisema

Mama Mariam ameeleza kuwa matatizo ya akili yanapelekea kujiua hasa kwa vijana ambao wana umri kati ya  miaka 15 hadi 25 jambo ambalo linapoteza nguvu kazi ya Taifa.

 Hata hivyo ameisisitiza jamii kuendelea kufanya mazoezi, kujiepusha na vitendo viovu kwa vijana ili kujiepusha na tatizo hilo.

Akitaja changamoto zinazowakabili  Mratibu wa huduma za afya ya akili Zanzibar Suleiman Abdi Ali amesema kuwa wanakabiliwa na upungufu wa Madaktari na waaguzi jambo ambalo linahatarisha usalama wao kutokana na wagonjwa kuwapiga.

Vilevile  Mratibu huyo amesema wanaomba  kumaliziwa jengo lao ambalo lilioko nyuma ya jengo wanalotumia ili waweze kufanya kazi kwa ufanisi zaidi pamoja na kutiwa lami eneo la ndani ambalo litawaondolea usumbufu wagonjwa wao.

Sambamba na hayo Mratibu ameomba kupatiwa usafiri na mafuta ya kutosha kwani kufanya hivyo kutawaondolea usumbufu hasa katika utoaji wa elimu ya kinga na afya.

Nao wafadhili kutoka Norwe wamefahamisha kuwa wataendelea kushirikiana na Hospitali ya Mnazimmoja kwa kuwapa  kipaombele na kuhakikisha kuwa tatizo la afya ya akili linaondoka Zanzibar.

Akitoa neno la shukurani Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Mnazimmoja Muhidini Abdi Mahamoud ameahidi kuyafanyia kazi na kutatua changamoto zinazowakabili kitengo hicho.

Maadhimisho ya afya ya akili Duniani hufanyika kila ifikapo Oktober 10 ambapo kaulimbiu ya mwaka huu ni “KUIFANYA AFYA YA AKILI KUWA NA MANUFAA KWA WOTE”



Wahudumu kitengo cha Afya ya Akili  wakifanya igizo maalum linalohusiana na changamoto zinazowakabili wakati wa Utekelezaji wa  kazi zao , wakati wa hafla ya maadhimisho ya siku ya Afya ya Akili yaliyofanyika huko Hospitali ya Magonjwa ya Akili Kidongochekundu Zanzibar.
Wahudumu kitengo cha Afya ya Akili  wakifanya igizo maalum linalohusiana na changamoto zinazowakabili wakati wa Utekelezaji wa  kazi zao , wakati wa hafla ya maadhimisho ya siku ya Afya ya Akili yaliyofanyika huko Hospitali ya Magonjwa ya Akili Kidongochekundu Zanzibar.
Wadau mbalimbali wa Afya wakifuatilia kwa makini hafla ya maadhimisho ya siku ya Afya ya Akili yaliyofanyika huko Hospitali ya Magonjwa ya Akili Kidongochekundu Zanzibar.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar Mhe, Saada Mkuya Salum akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa Afya mara baada ya kukamilika kwa maadhimisho ya siku ya Afya ya Akili Kidongochekundu Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.