Habari za Punde

Matukio ya Picha Ziara ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Mwinyi Nchini Oman

 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti  wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Ali Mwinyi leo jioni tarehe: 12 Oktoba, 2022 amehudhuria mkutano mkubwa wa jukwaa la Biashara lililowaleta pamoja wafanyabiashara na wawekezaji mbalimbali.

 Katika mkutano huo Rais Dk Mwinyi,  aliwahakikishia usalama wafanyabishara  wa vitega uchumi vyao kwani kwa sasa Zanzibar kisiasa imeimarika kisiasa baada ya mivutano ya muda mrefu hali iliyosababisha kuundwa kwa serikali ya Umoja wa Kitaifa.

Mh. Rais Dk Hussein Ali Mwinyi pia alitumia jukwaa hilo la wafanyabiashara kuutangaza uchumi wa buluu kwa kuwaalika  katika Utalii ukiwemo ule wa fukwe  utalii wa kujionea urithi wa kuvutia wa Zanzibar  ikiwemo utamaduni wake, na utalii wa michezo na mikutano mikubwa.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.