Habari za Punde

Elimu ya sera inahitajika kuelekea matumizi ya nishati safi ya kupikia

 NA MWANAJUMA ABDI, DAR ES SALAM


JOPO la watoa mada wamesema elimu ya sera inahitajika Kwa watanzania kuelekea matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia  hususani Kwa wanawake ili kujiepusha na magonjwa mbali mbali yanayosabishwa nishati zisizokuwa salama za Kupikia.

Hayo waliyasema jana, Dar es Salaam katika kongamano la kitaifa la Nishati Safi ya Kupikia wakati wakijadili mada ya sera, sheria, kanuni na mifumo ya udhibiti ya kuwezesha Nishati Safi ya Kupikia.
Walisema wanawake ndio waathirika wakubwa wa Nishati isiyosalama ya Kupikia katika kuandaa chakula na masuala mbali mbali ya kifamilia.

Mkurugenzi Mtendaji Envirocare, Loyce Lema alisema elimu ya sera inahitajika kwa wananchi hususani wanawake ambao waathirika , ambao ndio wanatafuta kuni, mkaa na Maji Kwa ajili ya Kupikia  pamoja na kutunzaji wa mazingira.

Alisema wanawake wamekuwa hawanga wakubwa katika kupata magonjwa yanatokana na Moshi na kusababisha kupata matatizo ya kifua, macho na maradhi mengine yanayotokana ma matumizi yasio sahihi ya Nishati ya kupikia .

Aidha alishauri serikali itafute nishati mbadala na kumuondoa mwanamke katika madhara ya kiafya licha ya kuja na matumizi ya gas na umeme.

Nae Prof. Ramanus Ishengama kutoka Chuo Kikuu Cha Kilimo Cha Sokoine alisema sera ya Nishati ya mwaka 2015 imeshindwa kutoa muelekeo wa uchaguzi wa mazingira katika masuala mazima ya Nishati Safi ni ipi.

Alieleza licha ya kuwa sera hiyo ni ya hivi karibuni lakini inahitaji kufanyiwa marekebisho ili isaidiane ma sheria kuweka asilimia 85 ya matumizi ya nishati ya kuni na mkaa.

Alisema ujio wa Nishati Safi ya Kupikia ikiwemo gas na umeme, lakini alisisitiza Kwa upande wa vijijini watatumia muda mfupi au miaka mingapi ili kukubaliana kutumia Nishati hiyo.

Nao wachangiaji mbali mbali walisema kila nyumba inazalisha gas inayotokana na taka taka hivyo walishauri serikali kikosi kazi kitachoundwa wafanye kazi ya Kupitia sera na utafiti ili waje ma majibu ya kuwepo Kwa Nishati mbadala Kwa vile baadhi ya mikoa Kuna baridi sana na watu wamezoea kuwacha kuni ili kuota moto na matumizi ya Kupikia.

Akitoa ufafanuzi wa mjadala huo, Waziri wa Nishati January Makamba alisema utunzi wa sera ni Kwa ajili ya kuimarisha mifumo katika sekta na Taasisi husika katika kukuza maendeleo ya nchi.

Alieleza mifumo ipi Bora ya kisera na kisheria itayowezesha kupatikana Kwa Nishati Safi ya Kupikia nchini Kwa kuanzisha mijadala na mitazamo ya kifalsafa, itikadi ili kuona rasilimali zinavyotumika ipasavyo Kwa lengo la kufikia mkakati endelevu katika suala hilo.

Alisisitiza kikosi kazi kitahusika na sera ya mkakati Kwa Kupitia maagizo ya Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan aliyoyatoa katika hotuba yake ya ufunguzi.

Alisema Kuna fursa nyingi za ajira katika Nishati Safi ya Kupikia, ambapo aliwatoa wasiwasi watu waliokuwa wamejikita katika biashara ya kuni na mkaa kuwa zipo kazi nyengine mzuri kuliko kukata miti na misitu ambayo ni rasilimali ya taifa katika maendeleo.

Akitoa mfano wa utengezaji wa mkaa kuwa Tani Moja ya mkaa inahitaji magogo ya miti Saba, hivyo watanzania wanaona jinsi gani rasilimali inavyopotea ma kusababisha uchafuzi wa mazingira kutoka kukata miti ovyo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.