Mkuu wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Karume Zanzibar (KIST), Dkt. Mahmoud Abdulwahab Alawi, wa kwanza (kushoto ) akipokea Tunzo ya Ushindi wa Maadhimisho ya kongamano la Sita la mambo ya TEHAMA (TAIC2022) kutoka kwa Mwanafunzi wa Taasisi ya Karume Abdi Salim Mohd aliyetokea mshindi wa kwanza katika kipengele cha Elimu, kulia ni Mkuu wa wasimamizi wa Project za Wanafunzi wa Taasisi ya Karume Yussuf Ali Said, hafla iliofanyika Ukumbi wa Mkutano wa Dkt. Idrissa Muslim Hija Mbweni Zanzibar.Mkuu wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Karume Zanzibar (KIST), Dkt. Mahmoud Abdulwahab Alawi akiwa katika Picha ya pamoja na Washindi wa Project mbali mbali kutoka Taasisi ya Karume pamoja na Wakuu wa Idara ya Taasisi hiyo katika Ukumbi wa Mkutano wa Dkt. Idrissa Muslim Hija Mbweni Zanzibar.
Picha na Maryam Kidiko – KIST.
No comments:
Post a Comment