Habari za Punde

Wawekezaji wakaribishwa Zanzibar Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imefungua milango kwa Wawekezaji wa Ndani na Nje ya Nchini katika Jitihada za kukuza na kuimarisha uchumi wa Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameyasema hayo katika Hotuba iliyomwa kwa niaba yake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla katika Uzinduzi wa Jukwaa la Biashara na Uwekezaji lililofanyika katika Ukumbi wa Golden Tulip Uwanja wa Ndege Jijini Zanzibar.

Amesema kuwa kuongezeka kwa Wawekezaji kutoka Ndani na Nje ya Zanzibar kutasaidia kufikia maendeleo jumuishi kiuchumi na kijamii ikijumuisha eneo la biashara huria katika Bara la Afrika ikiwa ni Miongoni mwa Miradi Mikuu katika Mfumo wa Maendeleo wa Afrika.

Amesema Serikali imekuwa ikifanyakazi kwa karibu na Sekta Binafsi ili kutoa Fursa pana  katika kuwaletea Maendeleo Wananchi wa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla ni dhahiri Uwekezaji unaofanywa unaotoka katika Taasisi za Fedha za Afrika unatafsiri kwa vitendo azma ya Serikazli ya Awamu ya Nane inayoongozwa na Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi.

“Lazima nikiri kuwa ninashauku kubwa sana ya kuona kuwa mawazo yenu, ufahamu wenu pamoja na mapendekezo yenu yanaweza kutumika katika kuboresha Zaidi mazingira mazuri ya Biashara na Uwekezaji hapa Zanzibar” amesema

Rais Dkt. Mwinyi amesema suala la kukuza Uwekezaji limekuwa moja ya Msingi wa Ajenda ya Maendeleo kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ikiwa inaenda sambamba na Sera ya Kitaifa ya kukuza uwekezaji hasa kupitia Uchumi wa Buluu.

Amesema Serikali imeanza kutekeleza Mradi wa kimkakati wa Uchumi,  Mradi wa Nishati Mbadala, Ujenzi wa Bandari ya Mangapwani, pamoja na Miundombinu ya Barabara.

 Aidha Rais wa Zanzibar ameeleza kuwa Serikali inaendelea kulinda Amani na utulivu uliopo nchini kwa kuwa na Muundo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa  kwa misingi ya utawala bora imedhamiiria kukuza uwekezaji kwa maslahi ya Wananchi wake wote.

 Sambamba na hayo Rais Dkt. Mwinyi amesisitiza kuwa licha ya kukumbwa kwa mripuko wa maradhi ya Uviko 19 bado Zanzibar inaendelea kuimarika katika Sekta ya Uwekezaji na Biashara ambapo miradi mbali mbali imeanzishwa imeweza kuzalisha ajira nyingi kwa Vijana.

Kwa upande wake Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Kazi, Uchumi na Uwekezaji Mhe. Madrik Ramadhan Soraga ameeleza kuwa Afrika inatanua wigo wa Soko la kukuza Biashara na Uwekezaji hatua ambayo inasaidia kukuza Seka hiyo Barani humo.

 Ameeleza kuwa Zanzibar inaendelea kutangaza Fursa mbali mbali za Uwekezaji  zilizopo ambapo Serikali imeweka Milango wazi kwa Wawekezaji kutumia Fursa hizo ili kukuza Uchumi wake hasa kupitia Fursa zilizopo katika Sekta ya Utaii na Miundombinu.

 Nae Muwakilishi wa Afrexim Bank Dkt. Gainamore Zanamwe ameonesha kufurahishwa kwake kwa fursa nyingi za kiuchumi zilziopo Zanzibar na kuahidi kutoa kipaumbele katika mipango yao ya mikopo nafuu katika kuunga mkono miradi mbali mbali Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.