Habari za Punde

Makabidhiano ya ripoti ya kuleta mapendekezo ya mageuzi ya mfumo wa Elimu

Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar  Lela Muhamed Mussa akizungumza na wajumbe baada ya kukabidhiwa ripoti ya kuleta mapendekezo ya mageuzi ya mfumo wa Elimu waliyofika  katika ukumbi wa mkutano wa wizara hiyo mazizini Zanzibar.
 Mwenyekiti wa kamati ya kikosi kazi profesa Idrisa Ahmada Rai akitoa maelezo  ya ripoti, ya  kuleta mapendekezo ya mageuzi ya mfumo wa elimu Zanzibar (kushoto) Waziri wa Elimu na Mafunzo ya amali Zanzibar Lela Muhamed Mussa.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya amali Zanzibar Lela Muhamed  Mussa akikabidhiwa ripoti na Mwenyekiti wa kamati ya kikosi kazi profesa Idrisa Ahmada Rai ya awamu  ya kuleta mapendekezo ya mageuzi ya mfumo wa elimu Zanzibar mara  baada ya kuwasilisha ripoti hiyo Ukumbi wa Wizara ya Elimu Mazizni Zanzibar.
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya amali Zanzibar  Ali Abdulgullam Hussein akitoa maelezo mara baada ya ripoti hiyo kuwasilishwa katika ukumbi wa Wizara ya elimu na mafunzo ya Amali Mazizini  Zanzibar (kulia) Waziri wa Elimu na Mafunzo ya amali  Lela Muhamed Mussa.

Baadhi ya wajumbe wa Kamati hiyo wakimsikiliza Mwenyekiti wa kamati ya  kikosi kazi  Profesa Idrisa Ahmada Rai (hayupo pichani) wakati akiwasilisha ripoti ya awamu ya kwanza ya kuleta mapendekezo ya mageuzi ya mfumo wa elimu Zanzibar.

Na Miza Othman - Maelezo Zanzibar.

Na Ali Issa Maelezo 12/12/2023.

WAZIRI wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Lela Muhamed Mussa amesema msingi wa mapendekezo ya  mageuzi ya elimu ni sekta ya kipekee ambayo inaangaliwa kwa umakini mkubwa ili kuleta mfumo wa elimu wenye manufaa kwa taifa .

Ameyasema hayo huko Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali wakati akipokea Ripoti ya awali ya kikosi kazi ya mapendekezo ya mabadiliko ya  mfumo wa wa Zanzibar utaotumika miaka 50 ijayo.

Amesema mabadiliko hayo ni yakumuwezesha mwanafunzi wakati anapomaliza masomo yake kwa kumpatia manufaa ambayo yatamsaidia katika harakati zake za maisha.

Waziri huyo alisema yaliotajwa katika ripoti hiyo ni yale ambayo serikali tayari yameshaanza kuyatekeleza,ikiwa ni pamoja na kuondoa uhaba wa madarasa,kupunguza idadi ya wanafunzi katika madarasa,na ujenzi bora wa majengo ya kisasa yanayozingatia watu wenye mahitaji maalumu.

Waziri alimshukuru mwenyekiti wa kamati hiyo ya kikosi kazi kwa ushirikiano wao kwa kuzitumia siku 60 vizuri bila kuchoka.

Alisema ripoti hiyo itapelekwa serikalini kwa kupatiwa Baraka  ili kuufanya mfumo wa elimu mpya kuwa na manufaa makubwa.

Nae Mwenyekiti wa Kamati ya Kikosi Kazi profesa Idrissa Ahmada Rai alisema ripoti hiyo waliipata kwa ushirikiano wa wadau wengi wakiwemo wazazi walimu ,wanafunzi wasomi wa dini na kupata nafasi ya kuona mifumo ya elimu ya nchi mbalimbali ikiwemo ,Kenya,Morishazi na nchi nyengine duniani,

Aidha alisema mfumo walioufanya nikumuwezesha Mzazibari kukabiliana na nchi za kiafrika ili kwenda sambamba na mabadiliko ya uchumi.

Hata hivyo alisema katika ripoti yao waliangalia masuala mengi yanayozoretesha elimu na kufeli wanafunzi ambazo walizibainisha baadhi nazo ni  udhaifu katika ufundishaji, baadhi ya walimu hawana sifa,walimu wanachelewa kufika skuli,walimu wakuu misaada yao midogo ya kuongoza Skuli,Wanafunzi wengi,uhaba wa madrasa,mfumo dhaifu wa elimu,wanafunzi wanarejea baada ya kufeli, maslahi duni ya Walimu,uhaba wa madawati na  kadhalika. 

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.