Habari za Punde

Rais wa Jamhuri ya Watu wa Sahrawi Atembelea Mji wa Serikali wa Mtumba Dodoma

 

Mkurugenzi Msaidizi wa Uratibu Bw. Omar S Ilyas, pamoja na Mratibu wa Mradi wa Ujenzi wa Mji wa Serikali w Mtumba Bw. Meshack Bandawe wakitowa maelezi ya Mradi wa Ujenzi wa Mji wa Serikali katika eneo la Mtumba Jijini Dodoma wakati wa ziara ya Rais wa Jamhuri ya Watu wa Sahrawi. Mhe. Brahim Ghali alipotembelea mradi huo na kuona maendeleo ya ujenzi wa mji wa Serikali Mtumba.

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Sahrawi, Mhe. Brahim Ghali leo amefanya ziara ndogo katika mji wa Serikali  Mtumba ambapo alitembelea jengo la Ofisi ya Rais Menejiment na Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

Katika ziara hiyo ndogo Mhe. Rais Brahim Ghali alikaribishwa na kuoneshwa Mji wa Serikali na Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu – Sera, Bunge na Uratibu ambaye ni Mkurugenzi Msaidizi wa Uratibu Bwn. Omar S Ilyas, pamoja na Mratibu wa Mradi wa Ujenzi wa Mji wa Serikali Bwn.  Meshack Bandawe, ambapo walipata nafasi ya kuonyeshwa kiwanja cha Ubalozi wa Taifa la watu wa Sahrawi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.