Habari za Punde

Diwani Kimaya Awataka Wazazi,Walezi Kuwapeleke Watoto wao Kituo cha Sayansi STEM PARK cha Jijini Tanga

Na Oscar Assenga.Tanga

DIWANI wa Kata ya Chumbageni (CCM) Ernest Kimaya amewataka Wazazi na Walezi Jijini Tanga kukitumia kituo hicho cha Sayansi STEM PARK kwa kuwapeleka watoto wao ili waweze kujifunza na kupata Ubunifu wa mambo ya Kisayansi ili baadae waweze kuwa wabunifu wazuri na wenye vipaji kwenye maisha yao.

Aliyasema hayo wakati wa ufunguzi wa kambi hiyo  Meneja wa Kituo Cha Sayansi STEM PARK TANGA wakati wa ufunguzi wa kambi maalumu ya kuwamejengewa Uwezo juu ya Sayansi ya Kilimo Cha Kisasa Maarufu kama Kilimo "Janja

Kambi hiyo  maalumu ambayo iliyofadhiliwa na Mashirika ya Club Rotary clubs Tanga , Robotech Labs na Tanzania Open Innovation(TOIO) kwa Ushirikiano wa Jenga Hub chini ya usimamizi wa Project Inspire ambao ndio wasimamizi wa Kituo Cha Sayansi Nchini STEM PARK kilichopo mkoani Tanga.

Alisema uwepo wa kituo hicho katika eneo lake umekuwa na tija kubwa kwani kimekuwa kikitumiwa na wanafunzi na Walimu kujifunza kwa vitendo masomo ya sayansi hivyo kusaidia wanafunzi wanapokuwa wakisoma kwa nadharia shuleni baadae wanapokwenda kwenye kituo hicho wanasoma kwa vitendo na hivyo kuwasaidia kuwa na uelewa mzuri wa mambo wanayofundishwa wakiwa darasani.

“Kwa kweli kituo hiki kinafanya kazi kubwa na nzuri sana hivyo niwapongeze kwani mafunzo mnayotoa vijana wetu ni mazuri na yanawasaidia namna ya kutumia ujuzi walioupata na hivyo kuepukana na kukaa vijiweni ambako wengine wanajikuta wakitumia dawa za kulevya “Alisema

Aidha alisema kwamba kazi inayofanywa na kituo hicho ni kubwa kwa sababu mafunzo waliyoyapata yanakwenda kuwasaidia kuwa wabunifu wazuri zaidi huku akiwataka pia kuyatumia vizuri kwa ajili ya tija zaidi.

Alisema kwamba mazoezi ambayo wamewafundishwa vijana hao watengeneze utaratibu mzuri baada ya wa kutoka hapo baadae waende kwenye uhalisi wakiondoka wanaondoka watakuwa kitu ambacho wanacho baada ya hapo vijana watakuwa na ujuzi mkubwa wa kuwatoa kwenye fikra.

Alieleza kwamba itawatoa kwenye fikra ambazo sio nzuri na badala yake watakuwa wabunifu na kuondokana na vijana wavuta bangi, madawa ya kulevya maana watakuwa wamejitambua na wanaamini wanafunzi wanashika sana wakiwa na umri mdogo.

Awali akielezea kambi hiyo Meneja wa Kituo cha Meneja wa Kituo Cha Sayansi STEM PARK TANGA  Max George alisema  Kituo hicho kimekuwa na utaratibu wa kuweka Kambi kwaajili ya kupata Mafunzo juu ya namna ya kutatua matatizo mbalimbali kwakutumia Sayansi,

Alisema kituo hicho kimekuwa na  utaratibu maalumu wa kuweka kambi kwaajili ya kupata mafunzo ya mada husika, kwa mfano Kambi hii tumeifanya kwa Wanafunzi wa Shule za Msingi Jijini Tanga kwaajili ya kujifunza Kilimo cha Kisasa changamoto mbalimbali za Kilimo Cha Kisasa Maarufu kama Kilimo Janja.

Aidha alisema lakini pia changamoto za kilimo kwa nyakati hizi sote tunafahamu kuwa ni mabadiliko ya Tabia Nchi ambayo yameperekea upungufu wa Mvua maeneo mengi, hivyo kwakupitia Kambi hii Wanafunzi wameweza kujifunza namna ya kulima Kilimo ambacho hakitahitaji maji mengi, wamejifunza jinsi ya kumwagilia mbegu lakini jinsi ya Kutumia mfumo wa mbolea na Umeme katika Kilimo" Alisema George

Alisema Kituo hicho kitaendelea kuwafundisha Wanafunzi masuala mbalimbali kisayansi nakuwataka Wazazi kuwaruhusu Watoto Wanapokuwa wanahitajika kituoni hapo,

"Kituo chetu kinafundisha Sayansi kwa ujumla na tutaendelea kuandaa Kambi kama hizi, Niwaombe Wazazi muwaruhusu Watoto wenu pale wanapohitajika lakini pia hata pale hatuwahiji ni vizuri Watoto mkawapatia utaratibu maalumu wa kumwezesha kufika kituoni kwaajili ya kujifunza Sayansi, hapa mwanafunzi anaruhusiwa kuja muda wote kujifunza na Walimu wapo muda wote " Alisisitiza George

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.