Habari za Punde

Kikao cha Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Sheria

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika na Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene leo asubuhi pokea Jedwali la Uchambuzi wa Sheria Ndogo kutoka kwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu Sheria Ndogo Mhe. Kilumbe Shabani Ng’enda Bungeni Mjini Dodoma.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika na Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene amewapongeza wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Sheria Ndogo kwa kazi kubwa ya kuchambua sheria Ndogo zilizowasilishwa katika mkutano wa tisa wa Bunge.

Waziri ameyasema hayo leo tarehe 20/01/2023 katika ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo inaisaidia Serikali ili iwezee kufanya mambo kwa kuzingatia haki na sheria.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika na Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene (kushoto) akizungumza baada ya kupokea Jedwali la Uchambuzi la Sheria Ndogo.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu Sheria Ndogo Mhe. Kilumbe Shabani Ng’enda (kushoto) akizungumza kabla ya kukabidhi Jedwali la Uchambuzi la Sheria Ndogo.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo wakiwa katika kikao wakati wa kukabidhi jedwali la Uchambuzi la Sheria Ndogo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.