Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akishuhudia baadhi ya wanafunzi wa shule za
msingi na vyuo vilivyopo mkoani Dodoma wakipanda mti aina kandokando ya
barabara ya Dodoma – Morogoro eneo la Ihumwa Jijini Dodoma wakati alipoongoza
zoezi la upandaji miti kusheherekea Maadhimisho ya Miaka 59 ya Mapinduzi
Matukufu ya Zanzibar leo tarehe 12 Januari 2022.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akipanda mti aina ya Msabuni katika shule ya msingi Msalato Jijini Dodoma wakati akiongoza zoezi la upandaji miti kusheherekea Maadhimisho ya Miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar leo tarehe 12 Januari 2022.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akizungumza na Viongozi, Wananchi pamoja na Wanafunzi wa Shule za Msingi, Sekondari na Vyuo mara baada ya zoezi la upandaji miti lililofanyika katika eneo la Ihumwa na Msalato Jijini Dodoma wakati wa Maadhimisho ya Miaka 59 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar leo tarehe 12 Januari 2022.
No comments:
Post a Comment