Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango leo tarehe 18
Januari 2023 akimsalimia na kumpa pole Bi. Prisca Joseph Nyanda mkazi wa
Kagongwa wilayani Kahama Mwanamke mwenye ulemavu aliyetelekezwa na Mume wake
akiwa na watoto wawili ambao hutembea nao katika baiskeli yake mtaani kutafuta
riziki na mahitaji ya watoto hao.
Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango leo tarehe 18
Januari 2023 akimsalimia na kumpa pole Bi. Prisca Joseph Nyanda mkazi wa
Kagongwa wilayani Kahama Mwanamke mwenye ulemavu aliyetelekezwa na Mume wake
akiwa na watoto wawili ambao hutembea nao katika baiskeli yake mtaani kutafuta
riziki na mahitaji ya watoto hao.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango amesema uamuzi wa Serikali
utakaofikiwa baada ya mashauriano ya kina yanayoendelea juu ya kuanzishwa kwa
Mfuko wa Bima ya Afya kwa wote utazingatia maslahi ya wananchi wote na hasa
wenye kipato kidogo kwa lengo la kumwezesha kila mwananchi kupata huduma bora
za afya na kwa gharama nafuu.
Makamu wa Rais amesema hayo wakati
akizungumza na wananchi wa eneo la Kagongwa wilayani Kahama akiwa ziarani
mkoani Shinyanga leo tarehe 18 Januari 2023. Aidha amesema Serikali inaendelea
kupokea maoni na ushauri wa watu mbalimbali kuhusu kuanzishwa kwa mfuko huo.
Pia Makamu wa Rais ameutaka uongozi wa mkoa wa Shinyanga kujipanga vizuri zaidi na kusimamia
ukusanyaji wa mapato ya Serikali kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizowekwa.
Amesema hajaridhishwa na taarifa ya Mkoa kuhusu ukusanyaji wa mapato ya ndani
ya halmashauri za Shinyanga.
Aidha Dkt. Mpango Napenda amewasihi wakaguzi wote wa Mkoa pamoja na Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC)
kukagua mabwawa yote ya taka suku mara kwa mara na kufanyia kazi mapema dalili
za mabwawa hayo kupasuka ili kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza kama
ilivyotokea katika eneo la mwadui mkoani humo. Vilevile amemtaka Mthamini Mkuu
wa Serikali kukamilisha uhakiki na uthamini wa mali na mashamba ya wananchi wa
mwadui walioathirika na bwawa la taka sumu kupasuka na kuwalipa haki zao haraka
iwezekanavyo.
Akiwa
katika eneo la Kagongwa,Makamu wa Rais ameagiza kutafutwa na kuchukuliwa hatua
mwanaume mmoja aliyejulikana kwa jina la Athuman Yusuph kwa kumtelekeza
mwanamke anayefahamika kwa jina la Prisca Nyanda ambaye ni mlemavu akiwa na
watoto wawili na hivyo kulazimika kutembea na watoto hao katika baiskeli yake
wakati wote akitafuta riziki na mahitaji ya watoto hao.
Makamu
wa Rais ametoa shilingi milioni tano wakati akiwaongoza wananchi na viongozi wa
eneo hilo katika kumchangia mama huyo fedha zitakazomwezesha kujikimu na
kufanya biashara. Zaidi ya shilingi milioni sita na laki nane zimepatikana
katika harambee hiyo pamoja na vyakula mbalimbali ikiwemo unga na mchele.
No comments:
Post a Comment