Habari za Punde

Michuano ya Kombe la Mapinduzi 2023 Kati ya Mlandege na Namungo Uwanja wa Amaan Unguja,. Mlandege Imeshinda Mchezo huo kwa Penelti 5-4

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe.Othman Masoud Othman akiwa katika picha ya pamoja na Waamuzi wa Mchezo wa Nusub Fainali ya Kombe la Mapinduzi Cup.Kati ya Timu ya Mlandege na Namungo Mchezo uliofanyika Uwanja wa Amaan Unguja.Timu hizo zimetoka Sare ya Bao 1- 1. 

Timu ya Mlandege imeshinda mchezo huo kwa penenti 5-4  na kufanikiwa kuingia Fainali na Timu ya Singida Big Star,mchezo wa fainali kufanyika Ijumaa,13, Januari 2023 katika Uwanja wa Amaan saa mbili na robo usiku.
Kikosi cha Timu ya Mlandege kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuaza kwa mchezo wao wa Nusu Fainali ya Kombe la Mapinduzi Cup 2023, na Timu ya Namungo mchezo uliofanyika Uwanja wa Amaan Unguja.Timu hiyo imetinga Fainali kwa kuifunga Timu ya Namungo kwa Penenti 5-4.
Kikosi cha Timu ya Namungo kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuaza kwa mchezo wao wa Nusu Fainali ya Kombe la Mapinduzi Cup 2023, na Timu ya Mlandege mchezo uliofanyika Uwanja wa Amaan Unguja.Timu hiyo imekubali kipigo kwa njia ya Penenti 5-4. wakati mchezo wa kawadi kutoka sare ya bao 1-1.
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.