Habari za Punde

Muuguzi asimamishwa kazi Hospitali ya Rufaa Mnazimmoja

Mwenyekiti Baraza la Wauguzi na Wakunga  Zanzibar Profess Amina Abdul-qadir Ali akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na hatua ya kusimamishwa kazi kwa  Mfanyakazi wa kada ya Uuguzi na Ukunga Wodi ya Wazazi Hospitali ya Rufaa Mnazimmoja aliemdharau mama aliefuata huduma ya kujifungua Hospitalini hapo,huko Wizara ya Afya Mnazimmoja , febuari 21,2023. PICHA NA FAUZIA MUSSA MAELEZO ZANZIBAR.
Mjumbe na Mwenyekiti wa kamati ya Maadili Baraza la Wakunga na Wauguzi Zanzibar (kulia) Zainab Hassan akitolea ufafanuzi juu ya maadili ya Ukunga na Uuguzi wakati wa mkutano wa Waandishi wa Habari uliohusiana na hatua ya  kusimamishwa kazi kwa Mfanyakazia wa kada ya Uuguzi na Ukunga Wodi ya Wazazi Hospitali ya Rufaa Mnazimmoja aliemdharau mama aliefuata huduma ya kujifungua Hospitalini hapo,huko Wizara ya Afya Mnazimmoja , febuari 21,2023. PICHA NA FAUZIA MUSSA MAELEZO ZANZIBAR.
Mwanasheria kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Zanzibar Salum Mohammed  Abdalla akitoa ufafanuzi wa kisheria kuhusiana na kwenda kinyume na Maadili ya kazi wakati wa mkutano wa Waandishi wa Habari uliohusiana na hatua ya kusimamishwa kazi Mfanyakazia wa kada ya Uuguzi na Ukunga Wodi ya Wazazi Hospitali ya Rufaa Mnazimmoja aliemdharau mama aliefuata huduma ya kujifungua Hospitalini hapo,huko Wizara ya Afya Mnazimmoja , febuari 21,2023. PICHA NA FAUZIA MUSSA MAELEZO ZANZIBAR.

Na Rahma Khamis Maelezo                      21/2/2023

Wauguzi na Wakunga hapa nchini wametakiwa kuwa na maadili mema na lugha nzuri wakati wanapowahudumia wagonjwa ili kuondoa malalamiko katika jamii.

Wito huo umetolewa leo katika Ukumbi wa Wizara ya Afya Mnazimmoja na Mwenyekiti wa Baraz la Wauguzi na Wakunga Zanzibar Prof Amina Abdulkadir Ali katika mkutano na Waandishi wa Habari kuhusiana na taarifa iliyotolewa na  mawiyo kuhusu Muuguzi wa Hospitali ya Mnazimmoja kutowajibika ipasavyo kwa mzazi aliefika hospitalini hapo kwa ajili ya kujifungua.

Amesema kitendo kilicho fanywa na muuguzi huyo si kitendo cha kiungwana kwani kimechafua mwenendo mzima wa wauguzi na kuitia doa hospitali jambo ambalo linarejesha nyuma jitihda za Serikali ya kuwapati huduma bora wananchi wake.

Amefahamisha kuwa miongoni mwa kazi za baraza la wauguzi na wakunga ni kupokea malalamiko kwa wananchi na kuyachunguza baadae kuchukua hatua ikiwemo kupewa onyo au kusimamaishwa kazi.

Prof Amina ameeleza kuwa katika hatua walizozichuka kwa mfanya kazi huyo ni kumsimamisha kazi kwa muda wa miezi sita bila ya malipo na endapo atafanya tukio jengine atachukuliwa hatua kubwa zaidi ikiwemo kunyang’anywa leseni ya kufanyia kazi sehemu yeyote.

Akizungumzia suala la nidhamu Prof huyo amesema baadhi ya wauguzi hawana maadili mazuri kwani lugha wanazotumia hazipendezi kwa mgonjwa kwani mgonjwa akenda kwake lazima amhudumie.

“iwapo mgonjwa ataletwa katika kitengo chako muuguzi au daktari alieyepangwa kazi ndie dhamana wa pale hivyo ni wajibu wake kumsaidia mgonjwa huyo kwa kumpatia huduma stahiki na endapo litatokea lolote juu ya mgonjwa basi atahusika,”alisema Mwenyekiti huyo.

Nae Mwanasheria kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Salim Khamis Abdala amesema kuwa wamechukua hatua hiyo kutokana na kuwepo kwa malalamiko mengi hasa katika kada hiyo.

Aidha amefahamisha kuwa kwa mujibu wa sharia kifungu no 23 baraza limepewa uwezo wa kumsimamisha kazi au barua ya onyo mfanya kazi yeyote alienda kinyume na maadili na sharia ya kazi.

Kwa upande wake Mjumbe ambae pia ni Mwenyekiti wa Maadili katika Baraza hilo Zainab Hassan amewashauri wafanya kazi kubadilika na kushirikiana kwa pamoja kati ya wauguzi na wahudumu kwa Imani ili kufikia malengo.

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.