Habari za Punde

Mhe Othman awatembelea wagonjwa Mkoa wa Kaskazini Pemba


 

MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman, amesema ugonjwa ni sehemu ya mitihani kutoka kwa mola muumba kuwapa waja wake ili wawenze  kumkumbuka.

Mhe Othman ameyasema hayo   kwa nyakati tofauti huko katika vijiji vya Kiuyu Maziwa N’gomba na Chamboni Micheweni Mkoa  Kaskazini Pemba alipowatembelea na kuwapa pole wagonjwa tofauti vijini humo.

Mhe. Othman amewataka wagonjwa hao kuendelea kuwa na subria  kwa ugonjwa walionao na kumuomba Mwenyezi Mungu awaponeshe  na kuwarejeshea afya yao haraka ili waendelee na shughuli zao za kwaida za ujenzi wa taifa.

Wagonjwa aliowatembelea ni Ndugu Ramadhan Saleh Faki wa Kijiji cha Maziwa N’gombe na ndugu Hamadi Fundi Kombo wa Chamboni Micheweni ambapo wanasumbuliwa na ungonjwa kupooza kwa zaidi ya  miezi saba sasa.

Nao wagonjwa hao walimshukuru Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar kwa kuwatembelea na kuwapa na kwamba jambo hilo linawapa moyo wa matumani kwamba viongozi wapo karibu na wananchi wanaowaongoza.

Wamesema kwamba suala hilo ni jema na linajenga imani kubwa kwa wananchi katika kushirikiana na viongozi wao katika masuala mbali mbali.

Wakati huo, Mhe. Othman alifika nyumbani kwa Marehem Habib Ali Mohammed Mkoroshoni Chake chake Pemba kwa aliyemkuwa Mwakilishi wa Jimbo la Mtambwe kuipa pole familia ya marehemu huyo kwa kuondokewa na baba yao.

Aidha Mhe. Othman pia alitembelea Familia ya Omar Khamis Haji  Katibu wa Tawi la ACT huko Kijiji cha Kwale chake chake Pemba kuipa pole kufuatia kifo cha Mzee wao Marehe Omar Khamis Haji aliyezikwa leo kijiji hapo.

Mhe Othman amewataka wanafamilia hao kuwa na subra katika kipindi hiki kigumu cha msiba na kuwataka kuendelea kumuombea dua marehemu kwa kuwa ni jambo pekee litakalomsaidia kupata radhi na msamaha wa mola muumba.

Nao wanafamilia hao walimshukuru Mhe. Othman kwa kufika na kuwapa pole wanafamilia hao kufuatia vifo  vya wapendwa wao. hapo juzi na kuzikwa jana huko Kijiji kwao Uwonde mtambwe.

Mharehem Habib Ali Mohammed aliyekuekuwa mwakilishi wa Jimbo la Mtambwe alifariki usiku wa kuamkia Ijumaa ya tarehe tatu Machi mwaka huu katika Hospitali ya  Saifee huko mjini Dare Es Salaam alikolazwa  kwa matibabu kufuatia kuangaka ghafula tokea Februari 21 mwaka huu akiwa katika shughuli zake za kuwatumika wananchi na kupoteza fahamu hadi mauti yalipomkuta juzi.

Mhe . Othman yupo kwenye ziara rasmi ya siku nne huko kisiwani Pemba  kushiriki katika shughuli za chama na Serikali.

Mwisho.

Mwisho Imetolewa na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar kupitia Kitedngo chake cha Habari leo tarehe 05/03/023.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.