NI MKUFUNZI DENIS KAYOMBO
Na.Adeladius
Makwega-MWANZA
Wafanyakazi
wa Chuo Cha Maendeleo ya Michezo Malya, mkoani Mwanza Aprili 13, 2023 wamemchagua
mkufunzi Denis Kayombo kuwa mfanyakazi bora kwa mwaka huu katika uchaguzi
uliwakusanya wafanyakazi wote wa kada mbalimbali kuelekea Siku ya Wafanyakazi
Duniani, Mei Mosi , 2023.
Akizungumza
mara baada ya kutangazwa mshindi mwalimu Kayombo alisema,
“Ninawashukuru
sana, maana niliamka asubuhi sikuwa na ili wale lile kujua kuwa leo nitachaguliwa
kuwa mfanyakazi bora. Asanteni sana kwa kuwa mmeona ninatosha na ninafaa. Mimi
na wezangu tuliokuwa katika kinyang’anyiiro hiki sote ni bora. Nilipokuwa
napiga kura nilijipigia mwenyewe kwa kuwa nilipendekezwa tu, nikiogopa kukosa
kura kabisa, angalau nipate kura hata moja, lakini kumbe wengine mmenipigia!
Tushirikiane kukipeleka mbele chuo chetu na kuyafanikisha maslahi mapana ya
michezo na taifa letu.”
Katika uchaguzi huo mkufunzi Silveli Hema
alipata alipata 6.7% ya kura zote, mkufunzi Idd Luswaga alipata 33.3% ya kura
zote na huku mkufunzi Denis Kayombo aliyeshinda alipata 60% ya kura zote.
Akizungumza baada ya kutangazwa matokeo hayo
mwakilishi wa TUGHE katika Baraza la Wafanyakazi Bi Rita Samweli alisisitiza,
“Tumeshafanya
uchaguzi na tumempata yule ambaye tunamuona ni sahihi kupata nafasi hii,
ninachoomba tuendelee kushirikiana, tuendelee kufanya kazi ili tuone
tunafanyaje kwa mwenzetu aliyeshinda. Tunawapongeza wote watatu mliopigiwa
kura, nyinyi ni wafanyakazi wetu bora lakini jina moja ndilo linalotakiwa.”
Kikao
hicho cha uchaguzi kilihitimishwa kwa mwakilishi wa wafanyakazi wa Chuo Cha
Maendeleo ya Michezo Malya katika Baraza la Wafanyakazi Wizarani mkufunzi mkuu
Joachim Maganga kutoa mrejesho wa Kikao cha Baraza la Wafanyakzi la Machi 2023.
No comments:
Post a Comment