Habari za Punde

Mabaraza ya Wazee wa Unguja Kuwaenzi Wazee ili kuhakikisha wazee wanaishi salama.

Na. Maulid Yussuf - WMJJWW.

Idara ya Ustawi wa Jamii na Wazee inaendelea kutoa Elimu juu ya namna ya kuwatunza na kuwaenzi Wazee kwa Mabaraza ya Wazee wa  Unguja ili kuhakikisha wazee wanaishi salama.

Mkuu wa Divisheni ya Maendeleo ya Wazee Bi Kame  Sheha Ussi amewaomba Mabaraza ya Wazee kuwaeleza familia katika shehia zao juu ya wajibu wao kwa Mzee wake, ikiwa  ni pamoja na kutoa upendo, huruma, chakula, hifadhi na matibabu pamoja na kuwahimiza juu ya kumuamudu Mungu kwa kila muda unapofika.
Pia amesema ni muhimu kumuwezesha kuishi na mwenza wake iwapo hamna sababu, kutoa msaada wowote unaofaa kila unapohitajika pamoja na kuendeleza umiliki wa mali zake.

Wakitoa maoni yao Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo  wameshauri Mabaraza ya wazee kusaidia Serikali katika kuwasaidia wazee kujua tarehe zao za kuzaliwa kwani baadhi  ya wazee wanakosa kupata haki zao hasa za Pensheni Jamii.

Aidha wamesema linapokuja zoezi la uhakiki kwa ajili ya Pencheni Jamii, wanapata usumbufu kwa baadhi ya wazee  kutojua tarehe zao halisi za kuzaliwa hivyo, ni vyema kushirikiana katika suala hilo ili nao waweze kupata haki zao.

Kuhusu suala la kuwashughulikia wazee,  washiriki hao wamesema kuna baadhi ya wazee wanakuwa wanakataa kuhudumiwa na watoto wao na wengine kujifanya ombaomba na kujiandikisha wenyewe katika nyumba za wazee, hali ambayo nayo pia inaweka unyonge watoto wake.

Nao Maafisa Ustawi wanaoshughulikia utoaji wa Pencheni Jami  bi Raya  Salim Abdallah na Bi mwajuma Kali wamewaomba Mabaraza ya wazee kuwasaidia kwa wazee wao katika Shehia zao kwani wanekuwa wakikabiliwa na changamoto mbalimbali wanapofika katika utoaji wa Pencheni hizo.

Wamedai kuwa kuna baadhi ya Maafisa wanapata maradhi ya kuanguka ghafla, na wengine kupoteza pesa bila ya kujijua kwa madai ya kuwepo kwa mazingara  yanayofanywa na wazee katika baadhi ya shehia.

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA UHUSIANO WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII JINSIA WAZEE NA WATOTO 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.