Habari za Punde

Ufunguzi wa Masjid El -Marhoum Abdel Moneim Shahein Kizimkazi Mkunguni Mkoa wa Kusini Unguja


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Viongozi wa Serikali na Mfadhili aliyejenga Masjid El Marhoum Abdel Moneim Shahein Kizimkazi Mkunguni Sheikh.Sharif Abdel Shahein, baada ya kuwasili katika viwanja vya Masjid hiyo kwa ajili ya ufunguzi wake uliofanyika 26-5-2023. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akiondoa pazia kuashiria kuweka Jiwe la Msingi la Ufunguzi wa Masjid El  Marhoum Abdel Moneim Shahein Kizimkazi Mkunguni Mkoa wa Kusini Unguja na akiwa na Mfadhili wa wa ujenzi wa Masikiti huo wa Masjid Abdulmonem Sheikh. Sharif Abdel Shahein kutoka Nchini Misri na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria, Utumishi na Utawala Bora Zanzibar.Mhe.Haroun Ali Suleiman na Mkuu wa Wilaya ya Kusini Unguja Mhe. Rajab Yussuf Mkasaba.  
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akikata utepe kuashiria kuufungua Msikiti wa Masjid El Marhoum Abdel Moneim Shahein Kizimkazi Mkunguni Mkoa wa Kusini Unguja  na (kulia kwa Rais) Mfadhili wa wa ujenzi wa Msikiti huo Sheikh. Sharif Abdel Shahein kutoka Nchini Misri na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mhe. Rashid Hadid Rashid na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria, Utumishi na Utawala Bora Zanzibar.Mhe.Haroun Ali Suleiman na Naibu Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Mahmoud Mussa Wadi.  

Mfadhili wa ujenzi wa Masjid masjid Al – Marhoum Abdel Moeim Shahein wa Kizimkazi Mkunguni Sheikh Sharif Abdel Shahein akizunhumza wakati wa hafla ya ufunguzi wa msikiti huo, uliofunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi.   

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.