Habari za Punde

Ziara ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Chongolo Wilaya ya Mufindi

Sehemu ya Wakazi wa Ikongosi  waliojitokeza kwenye kikao cha nje ambapo Mgeni Rasmi alikuwa Katibu Kuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akizungumza na wanachama na wanachi wa Nyololo waliohudhuria kikao maalum cha shina namba 27, Nyololo wilaya ya Mufindi, ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya siku 7 mkoani Iringa .
Sehemu ya wakazi wa kata ya Igowose waliojitokeza kumsikiliza Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo alipotembelea na kujionea maendeleo ya ujenzi wa Shule mpya ya Msingi ya Kisalasi inayojengwa na Serikali kupitia mradi wa BOOST.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa Ndugu Daud Yasin (kulia) na Mbunge wa Jimbo la Mufindi Kusini (CCM) Ndugu David Mwakiposa Kihenzile pamoja na Viongozi na wanachama wengine wakitembea kwa miguu kuelekea Nyololo kuhudhuria kikao cha shina namba 27, ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya siku 7 mkoani Iringa .

Katibu Mkuu ameongozana na Wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Katibu wa NEC Oganaizesheni Ndugu Issa Haji Ussi Gavu na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndugu Sophia Mjema.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Ndugu Halima Dendego (kushoto) kabla ya kuanza kwa kikao cha shina namba 27 lililopo Nyololo wilaya ya Mufindi, ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya siku 7 mkoani Iringa .

Katibu Mkuu ameongozana na Wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Katibu wa NEC Oganaizesheni Ndugu Issa Haji Ussi Gavu na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndugu Sophia Mjema.

 Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akiteta jambo na Katibu wa NEC Oganaizeshi Ndugu Issa Haji Ussi Gavu (kulia) wakati wa kikao cha nje na wakazi wa kata ya Ikongosi, Mufindi mkoani Iringa.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.