Habari za Punde

KIST Yapokea Mtaala wa Fani ya Uhandisi wa Vifaa Tiba Kutoka Chuo cha Ufundi Arusha

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Ali Abdulgulam Hussein amesema, lengo la Serikali ni kuhakikisha Elimu  ya Ufundi inapewa kipao mbele ili kuweza kuleta maendeleo katika kila sekta Nchini.

Amesema Hayo wakati wa hafla ya Makabidhiano ya Mtaala Mpya kwa Fani ya Biomedical Engineering Kati ya (KIST) na Ujumbe kutoka Chuo Cha Ufundi Arusha,  iliyofanyika Katika Ukumbi wa Mikutano wa Dkt. Idrissa Muslim Hija, Mbweni Zanzibar.

Amesema, fani za ufundi ni miongoni mwa fani ambazo zinawasaidia Vijana wengi kujiari wenyewe pasipo kutegemea ajira maofisini, jambo ambalo limewasaidia vijna wengi kupiga hatua katika maisha yao.

Alifafanua kuwa, fani za ufundi katika  ngazi ya Astashahada  na Shahada  ndizo  ambazo zinasidia Vijana kujiajiri na kuajirika katika sekta mbalimbali nchini, hivyo uanzishwaji wa fani mpya ya Biomedical Enginnering nayo pia itatoa fursa kwa vijana kujiajiri na kuajirika nchini.

Aidha Naibu Waziri huyo alitumia fursa hiyo kupongeza jitihada zinazofanywa na Taasisi ya Karume kwa kufanikisha upatikanaji wa Mtaala huo, na kuutaka uongozi wa Taasisi kuzidi kuitangaza Fani hiyo pindi tu itakapoanzishwa chuoni hapo.

Katika hatua nyengine, Mhe. Abdulgulam amesema, Serikali  imejipanga kujenga Vyuo mbali mbali vya Mafunzo ya Amali Zanzibar  ili kuhakikisha Wanasomesha Vijana wengi wanasoma fani za ufundi.

Mapema Mkuu wa Taasisi ya Sayansi na Teknlojia ya Karume (KIST) Dkt . Mahmoud Abdulwahab Alawi,  amesema, endapo fani ya Biomedical Engineering itaanzishwa katika Taasisi ya Karume, itasaidia kuondoa changamoto ya uhaba wa wahandisi wa vifaa tiba katika  hospitali mbalimbali nchini.

Amesema, Kupitia Ushirikiano huo baina ya KIST na ATC, manufaa makubwa yanaweza kupatikana katika sekta ya elimu hasa katika fani za ufundi.

Nae Mkuu wa Chuo Cha Ufundi Arusha Dkt. Mussa Chacha, amesema, uongozi wa Chuo cha Ufundi Arusha  Upo tayari kuendeleza Ushirikiano ili Kuhakikisha mtaala huo unafanikiwa,   na lengo la kuzalisha Wataalamu Bora wa Fani mbali mbali za Ufundi linafanikiwa.

Alieleza kuwa, Mtaala huo umeandaliwa kwa Kuhusisha Wadau Mbalimbali wa elimu ikiwa  lengo ni kuwawezesha Wahitimu Kuweza kutumia Ujuzi katika kuendeleza Maisha yao.

Aidha amesema, Chuo cha Ufundi Arusha Kinamkataba wa Hiari na Ushirikiano  na Taasisi ya Karume  katika Kuendeleza Sekta ya Elimu Nchini.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.