Baadhi ya
wananachama na wafuasi wa cha ACT Wazalendo wakiwasikiliza viongozi wao wa
kitaifa akiwemo Mwenyekiti Babu Juma Duni Haji , Makamu Mwenyekiti wa Chama
hicho kwa Upande wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman , walipohutubiwa huko
katika Viwanja vya Bumbwini Makoba leo tarehe 6 Agosti 2023 katika Mkutano wa
hadhara wa kukamilisha mzunguko wa mwanzo wa mikutano ya aina hiyo. Picha na
Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais.
Mwenyekiti
wa Ngome ya wanawake Taifa wa chama cha ACT – Wazalendo Pavu Abdalla Juma
akizungunza katika mkutano wa hadhara huko Bumbwini Makoba leo tarehe 6 Agosti
2023.
Makamu
Mwenyekiti wa ACT- Wazalendo Mhe. Othman Masoud Othman akizungunza katika
Mkutano wa hadhara huko katika viwanja
vya Bumbwini Makoba leo tarehe 06, Agosti, 2023 akiwa katika hatua ya
kukamilisha mzunguko wa kwanza wa mikutano ya hadhara ya chama hicho. ( Picha
na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais.
Mwenyekiti
wa Chama hicho Taifa Babu Juma Duni Haji akizungunza na wanachama na wafuasi wa
chama hicho katika mkutano wa hadhara uliofanyika huko Bumbwini Makoba Makoba
Kaskazini B Unguja leo tarehe 06, Agosti 2023.
MWENYEKITI
wa Chama cha ACT -Wazalendo Taifa ndugu Juma Duni Haji, amesema kwamba ni
muhimu wazanzibari kushirikamana kuwa wamoja ili kutengeneza hatma njema ya kizazi
cha Zanzibar katika kujenga ustawi wa masuala mbali mbali ya maendeleo yao.
Mwenyekiti
huyo ameyasema hayo alipozungunza katika mkutano wa hadhara wa chama hiyo huko
Bumbwini Makoba ukiwa ni mkutano wa kukamilisha mzunguko wa kwanza wa mikutano
ya aina hiyo tokea kuruhusiwa kwa mikutano ya kisiasa miezi michache iliyopita.
Amesema
wazanzibar wanapaswa kuwa wazalendo wa kweli wa nchi yao na kushikamana kwa
kuwachana na ugomvi na uhasama wa
wenyewe kwa wenyewe ambao umewachosha sana wanzanzibari kwa kuwa limekuwa
likijitokeza kila baada ya uchaguzi.
Amefahamisha
kwamba ni vizuri wazanzibar washikamane
kuendesha nchi yao kwa kuwa na uwezo na
mamlaka ya kuamua kwa pamoja mambo mbali
mbali yanayohusu maendeleo ya nchi yao kwa pamoja.
Akizungunzia
suala la maadili ameseama kwamba vijana wengi hivi sasa hawana maadili na hivyo
wamekosa mwelekeo jambo ambalo linahitaji wananchi kuungana
nguvu zao kwa pamoja katika kuwasaidia vijana kuwa na mwelekeo utakaosaidia kuchangia
vyema ujenzi wa nchi yao.
Naye Makamu
Mwenyekiti wa Chama hicho Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman, ambaye pia ni
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, amesema kwamba Baraza la Wawakilishi la
Zanzibar ni ngome ya wazanzibari na kwamba serikali inawajibu wa kusimamia
masuala yanayoamuliwa na kusimamiwa na chombo hicho kwa niaba ya wananchi.
Akizungunzia
suala la Muungano amesema kwamba sheria inayopitishwa Zanzibar kuhusu masuala
ya Muungano kwa mujibu wa Ibara ya 64 ya Katiba ya Jamhuri sheria hiyo huwa ni
batili.
Amefahamisha
kwamba mnasaba huo Sheria ya kuyaondoa mafuta na gesi asilia katika orodha ya
Mungano kuruhusu utafutaji wa uchimbaji wa mafuta na gesi asilia Zanzibar
haiwezi kuwa sahihi kwa vile inapingana na katiba ya Jamhuri.
Amewataka wananchi
kukiunga mkono chama hicho na kushikamana pamoja katika kuhakikisha kwamba kwa
pamoja wananchi na viongozi wanaitetea Zanzibar kupoata msalahi na haki zake
mbali mbali ndani ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Naye
Mwenyekiti wa Ngome ya Wanawake wa Chama hicho Taifa Pavu Abdalla Juma , amesema
kwamba wananchi wa Bumbwini hawapingani na uamuzi wa serikali wa kuwepo
uwekezaji katika ujenzi wa Bandari na shughuli nyengine za maendeleo, lakini
inahitaji watendewe haki kwa malipo ya ardhi na vipando vyao kwa thamani halisi ya
uwekezaji huo.
Amesema
kwamba wananchi wengi walioathirika na mradi huo wamelipwa malipo kidogo jambo
ambalo limeleta manunguniko kwa vile malipo waliyopata hayaendani na thamani ya
ardhi na vipando vilivyoathirika.
Ameitaka
serikali kukaa pamoja na wananchi wa kijiji hicho kutafuta namna bora ya
kuondosha manunguniko ya suala hilo ikiwa ni pamoja na kutumia utaratibu wa
wananchi kukodisha ardhi zao ili wanufaike zaidi kuliko ilivyo sasa.
Amesema
kwamba hakuna sababu wananchi kuchukuliwa aradhi na kulipwa malipo duni ingawa
suala la uwekezaji linaungwa mkono na watu wote, lakini alisisitiza kwamba
linahitaji kuwa na neema zaidi kuliko kuleta manunguniko.
6, Agosti , 2023.
No comments:
Post a Comment