Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui akimkabidhi zawadi ya kitabu cha Zanzibar Mwakilishi Mkaazi mpya wa Shirika la Afya ulimwenguni nchini Tanzania Dr Charles Sagoe-Moses alipofika wizarani kwa kujitambulisha.
Mwakilishi Mkaazi mpya wa Shirika la Afya ulimwenguni nchini Tanzania Dr Charles Sagoe-Moses akimkabidhi Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui alipofika wizarani kwa kujitambulisha.
Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui akiwa katika picha ya pamoja na Mwakilishi Mkaazi mpya wa Shirika la Afya ulimwenguni nchini Tanzania Dr Charles Sagoe-Moses na watendaji wa Wizara ya Afya huko Mnazimmoja Zanzibar
WIZARA ya Afya Zanzibar imesema itaendeleza mashirikiano yake na Shirika la Afya Ulimwenguni WHO katika kuimarisha huduma za Afya hapa nchini.
Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui amesema hayo huko ofisini kwake wakati alipomkaribisha Mwakilishi Mkaazi mpya wa Shirika la Afya ulimwenguni nchini Tanzania alipofika kwa kujitambulisha.
No comments:
Post a Comment