Wanafunzi wanaokaa kambi ya masomo wa Skuli ya Sekondari Fujoni wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukabidhiwa msaada wa vyandarua kutoka kwa Taasisi ya Maleria Education Foundation (MEF).
PICHA NA FAUZIA MUSSA
Na Fauzia Mussa Maelezo Zanzibar
Wadau wa elimu,wafadhili na wahisani wameombwa kujitokeza kusaidia Wanafunzi wanaokaa kambi za masomo kwa ajili ya Maandalizi ya mitihani ya Taifa ili kuunga mkono Juhudi za Walimu katika kuhakikisha Wanafunzi hao wanafaulu na kupata matokeo Bora.
Akizungumza mara baada ya kupokea msaada wa chakula na vyandarua kutoka kwa TAASISI ya Corea Culture Foundation for Zanzibar Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Fujoni Abdu Maulid Fidia amesema wanafunzi wengi wanashindwa kushiriki katika kambi hizo kutokana na Hali duni za maisha yao.
Alifahamisha kuwa jumla ya Wanafunzi 120 wanaotarajiwa kufanya mitihani katika Skuli ya Fujoni wamekosa fursa ya kushiriki katika kambi hizo kutokana na kutokumudu gharama za kujikimu hali inayopelekea wanafunzi hao kukosa fursa ya kushirikiana na wanafunzi wenzao katika masomo ya ziada.
"Tuna jumla ya wanafunzi 198 wanaotarajiwa kufanya mitihani ya taifa kwa mwaka huu,ni wanafunzi 68 tu ndio waliopo kambini hii ni kutokana na familia zao kutokua na uwezo wa kulipia gharama za kambi."alifahamisha
Alifafanua kuwa Kila mwanafunzi analazimika kulipia laki mbili na hamsini kwa ajili ya mahitaji ya chakula kuanzia mlo wa asubuhi hadi usiku kwa kipindi chote atakachokuwepo kambini ,hivyo msaada wa chakula kutoka kwa wadau na wahisani utawasaidia wale ambao hawamudu gharama za kambi kuweza kushiriki.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa TAASISI ya Corea Culture Foundation for Zanzibar (KCFZ) Master Kim amesema Lengo la msaada huo ni kuwasaidia wanafunzi hao kujikimu katika mahitaji ya chakula na kulinda Afya zao dhidi ya maleria.
Aidha alifahamisha kuwa TAASISI hiyo mbali na kufundisha utamaduni wa korea kupitia michezo lakini pia imekuwa ikisaidia masuala mbali mbali ya kijamii ikiwemo kutoa msada wa vyakula na kuchimba visima vya maji katika maeneo mbalimbali ya Zanzibar.
Mapema Wanafunnzi wa Skuli ya Fujoni waliishukuru TAASISI hiyo Zanzibar Kwa msaada huo na kuwataka kuendeleza kutoa misaada kama hiyo mara kwamara kwani chakula ni kitu kinachohitajika na kutumika katika maisha ya Kila siku.
Walisema endapo wadau na wahisani watatoa msaada wa chakula katika kambini kutasaidia walioshindwa kumudu gharama za kujikimu kuweza kushiriki masomo katika kambi hizo.
"Mazingira ya Fujoni yanazalisha mbu Sana tunashukuru Kwa msaada huu wa vyandarua utatuwezesha kusoma kwa amani na kutukinga Sisi na maambukizi ya malaria"walifahamisha wanafunzi hao
Wakati huo huo watendaji wa TAASISI ya Korea Culture Foundation for Zanzibar walitembelea eneo wanaotarajiwa kuwekeza Chuo cha michezo katika kijiji cha Fujoni mara utaratibu utakapokamilika.
No comments:
Post a Comment