Habari za Punde

Mafundi Gereji Wilaya ya Mjini wapewa wiki moja kuhama

Wilaya ya Mjini.

Mkuu wa Wilaya ya Mjini Rashid Simai Msaraka ametoa muda wa wiki moja kwa Wafanyakazi wa Gereji katika maeneo ya Mjini kuhama katika maeneo mbalimbali waliopo na kuhamia eneo la Chumbuni karakana walipopangiwa.

 

Akizngumza na Wafanyabiashara mbalimbali wa Gereji katika Wilaya ya Mjini amesema lengo la kuwahamisha Wafanyabiashara hao ni kutaka Mji uwe safi na kuvutia.

 

Amesema lengo la kuwahamisha wafanyabiashara hao ni kuweka mazingira mazuri ya Mji na kuwapatia eneo sahihi la kufanyia biashara zao bila usumbufu na kuchafua mazingira.

 

Ameeleza kuwa Gereji zimekuwa nyingi katika maeneo ya Mjini na kutapakaa kila sehemu jambo ambalo linasababisha uchafu na uchafuzi wa mazingira .

 

Aidha amewaomba Wafanyabiashara hao kutii agizo la Serikali ili kuweza kuufanya Mji kuwa safi na salama na kuepukana na matatizo yanayoweza kujitokeza ikiwemo maradhi.

 

Hata hivyo asemema Serikali imeamua kuwashirikisha Wananchi katika Zoezi hilo ili kuepuka mivutano inayoweza kujitokeza na kuwaomba Wananchi kuunga mkono zoezi hilo ili liweze kufanikiwa na kutimiza azma ya Serikali kuweka Mazingira safi.

 

Nao baadhi ya Wafanyabiashara hao wameipongeza Serikali kwa kufanya uamuzi huo kwani utasaidia kuweka Mji Safi na kuondosha utitiri wa Gereji zilizotapakaa katika maeneo ya Mjini.

 

Hata hivyo wameuomba uongozi wa Wialaya ya Mjini kuimarisha eneo hilo walilopelekwa ikiwemo kuweka huduma muhimu kwa binadamu kama vile vyoo ili kuondosha usumbufu unaoweza kujitokeza kwa Wfanyabiashara hao.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.