Habari za Punde

Mhe Othman ajumuika na waumini katika Sala ya Ijumaa Msikiti wa Mbuyuni mjini Unguja

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Alhaj Othman Masoud Othman akisalimiana na Imamu Mkuu wa Msikiti wa Mbuyuni, Sheikh Farid Hadi Ahmed
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Alhaj Othman Masoud Othman akijumuika na waumini katika sala ya Ijumaa Msikiti wa Mbuyuni leo
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Alhaj Othman Masoud Othman akisalimiana na Ustaadh Abdallah Issa alipofika Msikiti wa Mbuyuni kwa ajili ya kusali Sala ya Ijumaa leo

 Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Alhaj Othman Masoud Othman, leo Septemba 01, 2023 amejumuika na Waumini mbali mbali wa Kiislamu, katika Ibada ya Sala ya Ijumaa, iliyofanyika Msikiti wa Mbuyuni, uliopo Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini- Magharib, Unguja.

Ibada hiyo imeongozwa na Imamu Mkuu wa Msikiti huo, Sheikh Farid Hadi Ahmed.
Kitengo cha Habari
Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar
Septemba 01, 2023.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.