Habari za Punde

Tuweke Mifumo Mizuri ya Muungano Kati ya Wizara ya Afya na TAMISEMI

 

Na. WAF - Dodoma

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe amesisitiza umuhimu wa kuweka mfumo wa muunganiko kati ya Wizara ya Afya na TAMISEMI ili kuwa na muunganiko mzuri wa kujua idadi ya watumishi pamoja vifaa tiba.

Dkt. Magembe ameyasema hayo Septemba 7,2023 wakati wa mkutano wa kitengo cha huduma za uchunguzi wa magonjwa ukiendelea pamoja na wadau wa huduma za uchunguzi wa magonjwa uliofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma.

“Wizara ya Afya pamoja na TAMISEMI kwakweli tunahitaji kuweka mfumo mzuri wa muunganiko kati ya Wizara ya Afya na TAMISEMI ili kuwa na muunganiko mzuri wa kujua idadi ya watumishi pamoja vifaa tiba”. Amesema Dkt. Magembe

Aidha, Dkt Magembe amewaomba wadau hao kuendelea kusaidia kuimarisha mifumo yetu inayoweza kutambua baina ya wizara ya afya na TAMISEMI ili fedha zinazopatikana ziweze kutumika kwa ufanisi na kutatua changamoto za uchunguzi wa Afya kwa wananchi.

“Kwakweli wadau wetu tunawaomba muendelee kusaidia katika kuimarisha mifumo hii ili tuweze kujua na kuona fedha zinapopatikana lakini pia tujue namna zinavyotumika katika kutatua changamoto za wananchi”. Amesema Dkt. Magembe

Vilevile Dkt. Magembe amesema uchunguzi wa kisayansi ni taaluma inayohitaji ushirikiano wa karibu hivyo wadau wa huduma za uchunguzi wa magonjwa na kitengo cha huduma za uchunguzi wa magonjwa wanapaswa kukaa pamoja ili kuelewa nani anahitaji msaada na jinsi ya kushirikiana katika kutumia data nyingi zinazozaliswa.

Pia, amesema kuwa ni muhimu sana kuimarisha huduma za uchunguzi, haswa kuanzia ngazi ya Msingi, tunawaomba wadau wote kuwa na mtazamo wa Kisekta na kuwa wataalam ili iwezekane kuoatikana kwa majibu sahihi na kuepuka kuwachanganya wananchi.

“Tunaona kuna umuhimu mkubwa kwa wadau wetu kuanza na mtazamo wa Kisekta kuanzia ngazi ya msingi kwakuwa wananchi ndipo wanapoanzia kupata huduma hadi ngazi ya juu kwa kuimarisha huduma za uchunguzi”. Amesema Dkt. Magembe

Mwisho, Dkt. Magembe amesema Idara ya huduma za uchunguzi wa magonjwa inapaswa kutoa mwongozo katika kuhakikisha kuwa sekta zote zinashirikiana kwa ufanisi kwenye utafiti hadi utekelezaji.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.