Habari za Punde

Rais Dk Hussein Mwinyi arejea Zanzibar




 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amerejea Zanzibar akitokea Dodoma akiwa Dodoma ameshiriki kikao Maalum cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC).

Pia ameshuhudia hafla ya utiaji saini mikataba 3 ya uwekezaji katika Bandari ya Dar es Salaam kati ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Kampuni ya DP World ya Dubai iliyofanyika Ikulu, Chamwino leo tarehe 22 Oktoba 2023.
Katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume amepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe.Idrissa Kitwana na Viongozi wengine wa Chama na Serikali pamoja na vikosi ya Ulinzi na Usalama vya SMZ na SMT.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.