Habari za Punde

Uongozi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar wakutana na Balozi wa Tanzania nchini Korea
 Mhe Ali Abdulgulam Hussein naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar na ujumbe wake pamoja na watendaji wa Shirika la Good Neighbors Tanzania wakiendelea na ziara ya mafunzo nchini Korea, leo walipata fursa ya kutembelea ofisi za ubalozi wa Tanzania nchini humo na kukutana na Mhe. Balozi Togolani Edriss Mavura, maofisa wa Ubalozi na Viongozi wa Diaspora wa Tanzania walioko Jamhuri ya Korea.

Katika mazungumzo hayo Mhe. Balozi Mavura amepongeza juhudi zinazofanywa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na hususan Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kuimarisha ubora wa Elimu na kuahidi kuwa Ofisi yake itaendelea kuhakikisha kuwa Sera ya Diplomaisia ya Uchumi inaimarisha uhusiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na Jamhuri ya Korea inaleta matokeo chanya katika kuunga mkono juhudi za serikali katika mageuzi ya Elimu na kuimairisha uchumi wa buluu.
Aidha Mhe. Balozi amepongeza juhudi za Serikali ya Jamhuri ya watu wa Korea kupitia mashirika yake ya kimaendeleo KOICA na GoodNeighbors kwa kufadhili miradi mbalimbali ya kimaendeleo na kuwezesha ziara ya mafunzo akiamini washiriki watajifunza namna Jamhuri ya Korea ilivyopiga hatua kubwa kiuchumi kupitia mageuzi ya Elimu na Teknokojia.
Mhe. Balozi ameeleza kuwa kutokana na uhusiano mzuri uliopo kati ya nchi hizo mbili, Tanzania inatajwa kuwa nchi ya pili kati ya nchi 45 za bara la Afrika zenye uhusiano wa kidiplomaisia na Jamhuri ya Korea inayopokea fedha nyingi kutoka Jamhuri ya Korea Kupitia miradi mbalimbali ya maendeleo na uwekezaji katika sekta mbalimbali za kijamii na kiuchumi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.