Habari za Punde

Waziri Mhe. Jafo Aeleza Mikakati ya Serikali

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo amehimiza zoezi la usafishaji wa mitaro iliyopo katika miji mbalimbali ili majitaka yaweze kutiririka sehemu inayotakiwa.

Amesema hatua hiyo itasaidia kupunguza athari za mafuriko kwa kuwa majitaka yasiyostahili huziba mitaro hiyo baada ya mvua kunyesha.

Dkt. Jafo amesema hayo wakati akifafanua masuala mbalimbali kuhusu hifadhi ya mazingira kwenye kipindi cha Dakika 45 kinachorushwa na kituo cha televisheni cha ITV.

Amesema kuwa katika kuipa umuhimu agenda ya mazingira Serikali mwaka 2021 ilikuwa Sera ya Mazingira na mwaka 2022 Mpango wa Taifa wa Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira ambayo unashirikisha taasisi mbalimbali katika kuweka mazingira ya kuwa salama.

Ikumbukwe Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa utabiri kuhusu mvua kubwa zinazotarajiwa kunyesha kwenye baadhi ya mikoa nchini hivi karibuni hivyo Serikali inawaelimisha wananchi ili wasipate madhara.

“Tukumbuke kwamba tuna changamoto ya taka kuwepo katika maeneo yasiyostahili kwa mfano taka kuingia kwenye mitaro ya majitaka na kuifanya kuizba hivyo kusababisha mafuriko zinaponyesha mvua, nasi Serikali tumetoa maelekezo ya kuziondoa taka hizo,“ amesema.

Kwa upande mwingine Dkt. Jafo amezungumzia kuhusu Katazo la Mifuko ya Plastiki na kusema kuwakampeni hiyo inaendelea na imepata mafanikio kwa kuwa wananchi wamepata uelewa na kuanza kutumia mifuko mbadala kwa ajili ya kubebea bidhaa.

Ameongeza kuwa awali kulikuwa na changamoto ya chupa za plastiki ambazo hutupwa ovyo na sasa hivi zimekuwa ni malighafi kwa viwanda kwa ajili ya kurejelezwa.

Aidha, Waziri Jafo amesema kuwa dawa ya malalamiko ya ucheleweshaji wa vibali vya uwekezaji imepatikana kwa kuanzishwa kwa mfumo akitolea vibali vya taka hatarishi na Tathmini ya Athari kwa Mazingira (EIA).

“Vibali vya taka hatarishi na EIA kwa ajili ya uwekezaji zamani malamikio yalikuwa mengi kuwa vinachelkewa ndio maana tukaja na mfumo ambao kila hatua inaoenekana kuanzia mwanzo hadi mwisho,“ amesisitiza.

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.