Na Fauzia Mussa, Maelezo
Mwenyekiti wa Kikundi cha Think Tank Zanzibar Salma Haji Sadat amesema ipo haja kwa jumuiya zinazotetea haki za makundi maalum kuungana na kufanya kazi Kwa pamoja kwa maslahi ya makundi hayo .
Akizungumza na wadau wa kutetea haki za makundi maalum wakati akifungua mafunzo ya kuwajengea uelewa juu ya asasi za kiraia alisema hatua hiyo itasaidia Kuibua mambo mbalimbali yanayowakumba na kurahisisha upatikanaji wa haki za watu wenye ulemavu ,Wanawake na Vijana .
Alisema utafiti uliofanywa na TAMWA umeonesha kuwa kukosekana kwa nguvu za pamoja kumesababisha kukosekana haki zao za Msingi ikiwemo Elimu na Afya .
Hivyo mafunzo hayo yamelenga kuwapatia uelewa watetezi hao juu ya namna ya kushirikiana na asasi nyengne zinazofanya kazi moja ili kuyafikia malengo yaliyokusudiwa kwa haraka pamoja na kuelewa mbinu Bora za kutetea haki za makundi hayo na namna ya kuboresha umoja kwaajili ya utetezi.
Akiwasilisha mada juu ya asasi za kiraia mwezeshaji Almas Mohammed alisema mawasiliano, umoja na kutokata tamaa , ni miongoni mwa mbinu Bora katika kuyafikia malengo ya utetezi na kufanikisha kupatikana kwa haki za wenye ulemavu,vijana na Wanawake kwa haraka zaidi.
Mwezeshaji huyo alisema jumuiya hizo zimekua na nguvu ya kuwezesha umma juu kutatua shida mbalimbali na Kuwafanya wasio na sauti kuwa na sauti.
Hata hivyo asasi hizo zimekua zikisaidia kutoa mitazamo sahihi ya kisera na miradi pamoja na kufanya Tafiti zinazotoa taarifa zinazosaidia katika mambo mbalimbali Nchini.
Aidha alisema asasi nyingi hukabiliwa na uhaba wa vitendea kazi, uongozi,pamoja na rasilimali fedha.
Nao washiriki wa Mafunzo hayo wameziomba asasi za kiraia kuacha kufanyakazi kwa kutegemea ufadhili hali inayosababisha kuwekewa masharti kwenye miradi wanayotekeleza.
Mafunzo hayo ya siku mbili yameandaliwa na TAMWA Zanzibar kwa ufadhili wa foundation for civil society na kushirikisha asasi za kiraia zinazosimamia na kutetea haki za watu wenye ulemavu, Vijana na Wanawake.
No comments:
Post a Comment