Habari za Punde

Waziri Mhe.Haroun Afuta Ada ya Usajili wa Mtu Mmojammoja kwa Wasaidizi wa Sheria

Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi na Utawala Bora Mhe,Haroun Ali Suleiman akifunga Jukwaa la 3 la Msaada wa Kisheria Zanzibar na kutoa agizo la kufutwa kwa ada ya usajili ya mtu mmojammoja ya mwaka kwa wasaidizi wa sheria ,hafla   iliyofanyika katika Ukumbi wa Chuo Cha Utalii Maruhubi .


Na Fauzia Mussa ,  Maelezo 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi na Utawala Bora Mhe,Haroun Ali Suleiman ameagiza  kufutwa kwa  ada ya mtu mmoja mmoja ya  usajili  kwa wasaidizi wa sheria kwani kazi wanayoifanya ni ya kujitolea .

 

Akizungumza wakati akifunga jukwaa la 3 la mwaka la msaada wa kisheria alisema agizo hilo limekuja kufuatia Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kutambua na kutathmini Mchango unaotolewa na wasaidizi hao .

 

Alifahamisha kuwa awali wasaidizi wa sheria walikua wakilipa kiasi cha shilingi elfu 20 Kila mtu kwa  mwaka kama ada ya usajili hivyo kwa sasa ada hiyo imeondolewa rasmi.

 

Aidha alizitaka Taasisi zote zinazohusika na usimamizi wa sheria  kushirikiana  kwa pamoja kwa lengo la kuimarisha maslahi ya wasaidizi wa SHERIA sambamba na kuwapongeza wasaidizi hao kwa kazi kubwa wanayoifanya bila ya malipo.

 

Awali Waziri Haruna   aliwataka wadau hao  kuyatumia majukwaa hayo  ili  kufanya tathmini na  kuangalia mafanikio na changamoto wanazokumbana nazo katika  utekelezaji wa maazimio wanayojiwekea na kuzifanyia kazi.

 

Akiwasilisha maazimio yaliyofikiwa katika jukwaa la 3 la mwaka la msaada wa Kisheria Mkurugenzi wa Idara ya Katiba na Msaada wa kisheria Hanifa Ramadhan Said amesema katika  jukwaa hilo  jumla ya maazimio 9 yamewekwa na kutakiwa  kufanyiwa kazi na kuwasilishwa ripoti ya  utekelezaji wake katika jukwaa linalofuata.

 

 Aidha alisema katika jukwaa hilo wajumbe waliazimia kuhamasisha baadhi ya Taasisi hususani vyama vya wafanyakazi kuwa na utaratibu wa kutoa huduma za msaada wa kisheria kwa wanachama wake na kuweka wasaidizi wa sheria kwenye maeneo yao.

 

Vilevile jukwaa limeazimia kwa Skuli ya sheria Zanzibar  kuweka ulazima kwa wanafunzi wanaosomea uwakili kutumia muda katika kutoa msaada wa Kisheria kama sehemu ya mafunzo  kwa vitendo, pamoja na  kuchapisha tafiti za Kitaifa kuhusu utoaji wa huduma za kisheria Zanzibar

 

Pia Jukwaa hilo  kupitia OR ,Katiba,Sheria Utumishi na Utawala bora lilizamiria kuanzisha na kusimamia kanzi data ya Kitaifa  na mfumo jumuishi wa kidijitali wa ukusanyaji taarifa za msaada wa kisheria   kwa kushirikiana na watoa huduma za msaada wa kisheria

 

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu OR Katiba Sheria utumishi na Utawala Bora Omar Haji Gora alisema jukwaa hilo linaendelea kuimarika siku hadi siku na kuahidi kushirirkisha washiriki kutoka nje ya Tanzani katika majukwaa yajayo.

 

Nao baadhi ya Wasaidizi wa Sheria walisema wamefurahishwa na kulipokea vyema agizo hilo linaloenda kuongeza nguvu ya wao kuendelea kufanya kazi hiyo ya wito.

Mkurugenzi Idara ya Katiba na Msaada wa kisheria Hanifa Ramadhan Said akisoma maazimio ya jukwaa la tatu wakati wa Hafla ya ufungaji wa jukwaa hilo iliyofanyika ukimbi wa Chuo cha Utalii Maruhubi Mjini Unguja.
Naibu Katibu Mkuu (OR), Katiba,Sheria, utumishi na Utawala Bora  Omar Haji Gora  akimkaribisha Waziri wa Nchi   (OR), Katiba,Sheria, utumishi na Utawala Bora  Haroun Ali Sleiman  kufunga jukwaa la 3 la mwaka la msaada wa kisheria lililofanyika Ukumbi wa Chuo Cha Utalii Maruhubi .

Washiriki wa Jukwaa la 3 la mwaka la Masaada wa kisheria wakifuatili hafla ya ufungaji wa jukwaa hilo huko Ukumbi wa Chuo Cha Utalii Maruhubi .

 Picha na Fauzia Mussa --Maelezo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.