Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano
na Mazingira) Mhe. Dkt Selemani Jafo akikabidhi Tuzo ya ‘Wanawake
katika Uongozi’ kwa Baraza la Wanawake Wafugaji (PWC) Tanzania, mshindi
wa kwanza kati ya washindani 500 dunia iliyotolewa na Taasisi ya Global
Centre on Adaptation (GCA) kwa Kiongozi wa Baraza hilo kutoka jamii ya Kimasai Bi.
Maanda Ngoitiko jijini Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu ambako unafanyika Mkutano
wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP28).

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt Selemani Jafo amekabidhi Tuzo ya ‘Wanawake katika Uongozi’ kwa Baraza la Wanawake Wafugaji (PWC) Tanzania baada ya kuibuka mshindi wa kwanza kati ya washindani 500 kutoka nchi mbalimbali dunia.
Tuzo hiyo imetolewa na Taasisi ya Global Centre on
Adaptation (GCA) jijini Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu ambako unafanyika Mkutano
wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP28).
Akikabidhi tuzo hiyo kwa Kiongozi wa Baraza hilo
kutoka jamii ya Kimasai Bi. Maanda Ngoitiko aliyeipokea kwa niaba ya Baraza
hilo, Dkt. Jafo amewapongeza kwa kuipatia Tanzania sifa.
“PWC wameiheshimisha sana Tanzania na kuifanya isikike
duniani na nina uhakika kabisa tuzo hii imetokana na juhudi binafsi za dada
yangu Maanda za kuimarisha uwezo wa uongozi wa wanawake wafugaji kwa kuwajengea uwezo kiasi
cha kufikia usawa katika kutoa maamuzi katika jamii zao,” amesema Waziri
Jafo.
Akishukuru kwa tuzo hiyo Bi. Maanda amesema kuwa Baraza
hilo linawahudumia wanawake na wasichana kutoka jamii za Wamasai, Sonjo, Akie
na Barabaig.
Ameongeza kuwa PWC ni shirika lisilo la kiserikali
linalofanya kazi kaskazini mwa Tanzania kufikia usawa wa kijinsia na maendeleo
ya jamii kupitia uwezeshaji wa wanawake na wasichana wa Kimasai.
Wakati huo Tanzania inaendelea kushiriki katika
Mkutano wa COP 28 sanjari na mikutano ya pembezoni (side events), mikutano ya
uwili (bilateral meetings) na warsha ambapo watu zaidi ya 81,000 kutoka
nchi zaidi 190 wanahudhuria.
Tanzania imeandaa banda la maonesho katika viwanja vya
Dubai Expo City likisheheni wizara na taasisi mbalimbali ambapo Ofisi ya Makamu
wa Rais inawakilishwa na Waziri Dkt. Selemani Jafo, Katibu
Mkuu Bi. Mary Maganga na wataalamu kutoka Ofisi hiyo.
Aidha, Mkutano huo unaochagizwa na kaulimbiu ya kitaifa ‘Kuimarisha Kilimo Himilivu na Uchumi wa Bluu
katika Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi‘, ulifunguliwa rasmi
Novemba 30 na unatarajiwa kuhitimishwa Desemba 12, 2023.
No comments:
Post a Comment