Habari za Punde

Na Mwandishi Wetu

TAASISI ya Tanzania youth Icon imetilaiana saini ya mkataba wa ujenzi wa uwanja wa Michezo Alabama na kampuni ya Sky City ambayo ndio itakayojenga uwanja huo, uliopo katika jimbo la Kikwajuni Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, unaodhaminiwa na mbunge wa jimbo hilo Mhandisi Hamad Yussuf Masauni.

 

Hafla ya utiaji saini mkataba huo ilifanyika huko katika skuli ya Dk. Ali Mohamed Shein Rahaloe mjini hapa, ambapo kwa upande wa TAYI aliesaini ni Mwenyekiti wake Abdalla Miraji na kwa SKY City iliwakilishwa na Abrahman Mohammed Said.

 

Akizungumza mara baada ya utiaji wa saini hiyo ulioenda sambamba na makabidhiyano ya hundi ya shilingi milioni 200,  Mwenyekiti wa TAYI Abdalla Miraji alisema kuwa ujenzi wa uwanja huo utagharimu shilingi  bilioni 1.7 na utachukuwa kwa muda wa miezi 18 hadi kukamilika kwake.

 

 

Alisema kukamilika kwake kutatoa fursa kwa vijana waliomo ndani ya jimbo hilo na nje ya jimbo hilo kukuza vipaji vyao.

 

Aidha alisema kuwa uwnaja huo utakuwa kichochoeo kikubwa cha kuibua vipaji mbali mbali vya michezo katika jimbo lao la Kikwajuni na Zanzibar kwa ujumla.

 

Alisema kuwa wakati wanaelekea katika harakati za uwanja huo wanahitaji na wao kujipanga kw akujengewa uwezo wa uendeshaji wa uwanja.

 

“Hili tunakuomba mheshimiwa Waziri kwani kiwanja kitamalizika na kuhitaji watalamu wa kukiendesha na sisi hatuna utaalamu mkubwa kwa hivyo tunakuomba ututafutie njia ya kupata mafunzo ya uendeshaji wa kiwanja na uongozi ili kikimalizika vijana wa TAYI waweze wenyewe kukiendesha na sio kutafuta watu kutoka mbali”, alisema.

 

Alisema kuwa kiwanja hicho kitakuwa cha kisasa chgenye teknolojia mpya, hivyo ni vyema serikali kupitia wizara ya Michezo kutafuta njia mbali mbali za kupata mafunzo ya uendeshaji wa uwanja na uongozi.

 

Mapema Mbunge wa jimbo hilo Mhandishi Hamad Yussuf Masauni alisema kuwa kukamilika kwa kiwanja hicho kutaifanya taassisi hiyo zile changamoto ambazo walikuwa wakizikabili kuzipatia ufumbuzi.

 

Hata hivyo alisema kuwa kuwepo kwa uwanja huo ndani ya jimbo hilo kutawaepusha vijana wao wengi kujiingiza katika makundi maovu kwani watapata nafasi za ajira za kuweza kujipatia kipato.

 

Sambamba na hayo alisema kuwa wananchi wa jimbo hilo ni mfano wa watu wenye kupenda maendeleo na ndio maana hvikwazo vya watu wachache wasiopendelea maendeleo hayo havijawaathiri.

 

Kwa upande wake Waziri wa Wizara ya Vijana, Habari, Utamaduni na Michezo Tabia Maulid Mwita aliwapongeza viongozi wa jimbo hilo kwa kusimamia vyema ilani ya CCM  katika jimbo lao.

 

Alisema kuwa viongozi hao wameonesha jitihada mbali mbali za kuleta maendeleo ndani ya jimbo lao ikiwemo sambamba na kuimarisha michezo jimboni humo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.