Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Mwinyi Azungumza na Wazee wa Mkoa wa Kusini Unguja

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akifurahia jambo wakati akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud na Mkuu wa Wilaya ya Kusini Unguja Mhe Galos Nyimbo, alipowasili katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kusini Unguja kwa ajili ya kuzungumza na Wazee wa Mkoa wa Kusini Unguja.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi  akizungumza na Wazee wa Mkoa wa Kusini Unguja katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kusini Makunduchi, wakati wa ziara yake na kuhudhuria Dua Maalum iliyoandaliwa kwa ajili ya kuwaombea Viongozi Wakuu na kuiombea Nchi Amani, iliyofanyika katika  Msikiti Mkuu wa Ijumaa Mtegani Makunduchi
WAZEE wa Mkoa wa Kusini Unguja wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) wakati wa ziara yake katika Mkoa huo mazungumzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kusini na kuhudhuria Dua Maalum ya kuwaombea Viongozi na kuiombea Nchi Amani,  iliyofanyika katika Msikiti Mkuu wa Ijumaa Mtegani Makunduchi
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akikabidhiwa zawadi maalum ya migomba na Kiongozi wa Wazee wa Mkoa wa Kusini Unguja Mzee Mwita Masemo Makungu (kulia kwa Rais) baada ya kumaliza mazungumzo yake na Wazee wa Mkoa huo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kusini Unguja Makunduchi leo 16-12-2023 na (kushoto kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.