Habari za Punde

Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Mhe. Omar Shaban Azungumzia Maendeleo ya Biashara na Viwanda Miaka 60 ya Mapinduzi

Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar Mhe. Omar Said Shaaban akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusiana na maendeleo ya wizara yake katika miaka 60 ya Mapinduzi huko Karume house Mjini Unguja.

Na Ali Issa - Maelezo Zanzibar.

Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Omar Said Shaban amesema Serikali itaendelea kufanya juhudi mbalimbali za kuhakikisha kwamba sekta ya viwanda inaimarika Nchini.

 Akizungumza na waandishi wa habari  kuhusu mafanikio ya wizara yake huko Karume house  amesema serikali imeweka maeneneo malumu kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda ili kutunza mazingira na kulinda afya za Wananchi.

Akielezea kuhusu maeneo hayo Mhe Waziri  alisema ni pamoja na eneo la Pangatupu na Dunga kwa upande wa Uunguja na eneo la Chamanangwe kwa upande wa Pemba.

Alisema muundo wa sera ya sekta ya viwanda katika miaka ya 2000 umebadilika kwa kiasi kikubwa ambapo sekta hiyo inaundwa na wazalishaji wagowadogo wakiwemo wajasiria mali

“kwamujibu wa sensa ya viwanda iliofanywa mwaka 2012 ilibainisha kuwepo kwa miradi ya uzalishaji 2,201ilitawanyika katika sehemu mbalimbali mikoa ya unguja na pemba”alisema waziri huyo.

Waziri huyo alisema kuwa katika kipindi cha mwaka 2022 uzalishaji wa viwandani umeongezeka ukilinganisha na mwaka 2021 ambapo unga wangano umeongezeka kutoka tani 35,513 kwa mwaka 2021mpaka tani 36,843,

Aidha alieleza kuwa uzalishaji wa mikate viwandani umeongezeka kutoka 237,918 kwa mwaka 2021 hadi 239,242 kwa mwaka 2022.

Alisema kuwa serikali imefanya mabadiliko kadhaa ya sera na sharia ya leseni namba 3 ya 1983, sharia ya biashara namba 4 ya 1989,sharia ya biashara no 4 ya 1989,sharia ya ushindani na kumlinda mlaji, no 2 ya 1995 sheria ya mizani na vipimo no 4 ya 1983,sharia ya chakula na ,madawa na vipodozi na 2 ya 2006.

Akizungumzia mafanikio kwa sekta ya biashara amesema Wizara kupitia tasisi ya viwango ZBS imeweza kupata ithibati ya ubora kupitia mfumo wa usimamizi kwa kiwango cha ISO 9001:2015

Aidha alifahamisha kua Wizara imekamilisha  uimarishaji wa mifumo ya usajili pamoja na kuunganisha mfumo wa mali Bunifu kupitia wakala wa usajili Biashara na mali ili kuweza kuhakikisha taasisi inatoa mazingira mazuri urahisishaji na urasimishaji wa biashara hapa Zanzibar.

Aidha alisema kuwa Serikali imefanikiwa  kuongeza bei ya karaafuu kutoka shilingi elfu  12000 hadi kufikia elfu  13000 kwa leo la kuinua kipato kwa wakulima.

Mkutano huo na Waandishi wa habari ulilenga kujadili mafanikio ya Wizara ya Biashara na maendeelo ya viwanda kuelekea MIAKA 60 YA MAPINDUZI.
Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar Mhe. Omar Said Shaaban akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusiana na maendeleo ya wizara yake katika miaka 60 ya Mapinduzi huko Karume house Mjini Unguja.
Mwandishi wa habari gazeti la habari leo Ligwa Paul akiuliza swali kwa Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar Mhe. Omar Said Shaaban wakati akitoa taarifa ya maendeleo ya Wizara yake kuelekea miaka 60 ya Mapinduzi huko Karume house Mjini Unguja.
Mwandishi wa habari  Bahari Fm Khadija Juma akiuliza swali kwa Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar Mhe. Omar Said Shaaban wakati akitoa taarifa ya maendeleo ya Wizara yake kuelekea miaka 60 ya Mapinduzi huko Karume house Mjini Unguja.

Afisa habari idara ya habari maelezo Zanzibar Ali Issa akiuliza swali kwa Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar Mhe. Omar Said Shaaban wakati akitoa taarifa ya maendeleo ya Wizara yake kuelekea miaka 60 ya Mapinduzi huko Karume house Mjini Unguja.

PICHA NA FAUZIA MUSSA-MAELEZO ZANZIBAR.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.